Na Mwandishi Wetu, Same

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kumtafuta Isaya Malogozi (anaedaiwa kuwa mwekezaji) ambaye amekaidi kuhudhuria mkutano wa hadhara kutakiwa kutolea ufafanuzi taarifa zake kutaja baadhi ya viongozi wa Wilaya hiyo akiwahusisha katika mgogoro wa ardhi wa muda mrefu baina yake na wanchi.

Pia amewataka Polisi kuachana na tabia ya kuwakamata baadhi ya wananchi katika kijiji hicho kwa madai ya kuagizwa na Issaya Malongoza (anaedai kuwa mwekezaji) mwenye mgogoro na wananchi wa kijiji hicho tangu mwaka 2016.

Ametoa maagizo hayo wakati wa mwendelezo wa ziara zake kusikiliza na kutatua Kero mbalimbali za wananchi katika Wilaya ya Same ambapo mara hii ziara hiyo imefanyika katika kijiji cha Nasuro kata ya Bangalala.

Mgeni ametumia nafasi hiyo kumtaka Malongoza (Mwekezaji) kuacha kufanya shughuli yoyote kijijini hapo mpaka kesi aliyoikatia rufaa na aliyoifungua wilayani kumalizika huku akisisitiza Polisi kumtafuta popote alipo kwa ajili ya kutoa maelezo ya kukaidi kufika kwenye mkutano.

"Mwekezaji huyu alitakiwa aje kwenye mkutano wa hadhara kutoa ufafanuzi kwa kauli zake zikiwemo za kawataja viongozi wa Wilaya amewaweka mfukoni na hakuna atakae mgusa wilayani hapa."

Awali akitoa ufafanuzi mgogoro baina ya wananchi na mwekezaji huyo Mwanasheri wa Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Upendo Kivuyo amesema mwekezaji alienda kijiji jirani cha Bangalala kuomba kuuziwa ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Amesema lakini Serikali ya kijiji hicho ikauza eneo la kijiji jirani(Nasuro) chenye mgogoro, badala ya kijiji alipo omba. "Huyu alishafunguliwa kesi ya uvamizi baraza la ardhi la Wilaya na kijiji kikashinda kesi hiyo.

" Hata hivyo mwekezaji alikata rufaa huko pia kijiji kikashinda lakini amekua akiendelea kuwatesa wananchi kwa kukata rufaa hata sasa kuna kesi iko mahakamani,"amesema.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema tayari katika kesi aliyofungua mwekezaji huyo Mahakama ya Mwanzo, wananchi wawili wamefungwa kifungo cha miezi sita kwa kosa la kuvamiwa eneo hilo ambalo kimsingi wamedai halikuuzwa na kijiji husika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...