WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amevitaka viwanda vyote nchini kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa gharama nafuu ili ziweze kuingia katika soko Eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA)
Ameyasema hayo Agosti 3, 2023 alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji wa maziwa na kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo.
"Serikali ya Awamu ya Sita inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wafanyabiashara na wawekezaji wanakuwa na mazingira bora na wezeshi ili kufanya biashara kwa tija na kukuza uchumi wa Taifa, " amesema.
Pia amesema Serikali ya Dkt Samia nikuona wafugaji wanabadilika kutoka katika ufugaji wa kienyeji kwenda katika uwekezaji wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya soko.
Aidha amepongeza kiwanda hicho kwa ajira walizotoa hapa nchini na ametaka ajirasizizo za moja kwa moja ziongezeke.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...