*Aishauri TIA kwenda katika mabadiliko ya kuwajengea ujuzi wataalam
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Festo Dugange amesema kuwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)ni Taasisi muhimu kwa Tamisemi katika miradi inayotekelezwa na Serikali.
Hayo ameyasema Dkt.Dugange wakati alipotembelea banda la TIA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Dkt.Dugange amesema kuwa katika Halmashauri ndipo mapato yanatoka ambapo TIA ndio wazalishaji wa rasilimali hiyo ya kusaidia serikali kuwa wataalam wa kukusanya mapato hayo.
Aidha amepongeza kuanzisha mfumo wa kufatilia mapato ambao utazinduliwa hivi karibuni na kutaka Tamisemi nayo ipate mafunzo ya kutumiw mfumo huo kwa ajili ya kwenda kutumika katika Halmashauri.
Dkt. Dugange amesema kuwa katika utoaji elimu waendane na kujenga ujuzi kwa vijana kutokana na mabadiliko yanayobadilika kila wa wakati.
Nae Makamu Mkuu wa Taaluma, Tafiti na Ushauri wa TIA Dkt.Momole Kasambala amesema kuwa TIA itaendelea kutoa elimu inayokidhi kwa mahitaji ya sasa ambapo wamekuwa wakifanya kupata matokeo chanya.
Dkt.Momole amesema kuwa TIA inatoa elimu ya ujasiriamali katika kufikia vijana wengi waweze kuingia katika sekta zingine na kuendesha maisha bila kutegemea sekta rasmi ambayo ni kuajiriwa serikalini .
Naibu Waziri wa Tamisemi Dkt.Festo Dugange akizungumza katika banda la TIA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Tamisemi Dkt.Festo Dugange akipata maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo wa Taaluma , Utafiti na Ushauri wa TIA Dkt.Momole wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TIA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mhadhiri wa TIA Baraka Kamwela akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itende Mbeya wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la TIA Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea viwanja vya John Mwangale jijini Mbeya.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa TIA , Lilian Rugaitika akizungumza na Shule ya Sekondari Itende Mbeya wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la TIA Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea viwanja vya John Mwangale jijini Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...