Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) CPA Golden Kajaba amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Shirika lilikuwa na lengo la kukagua vyama 5000 lakini tulikagua vyama 3878 sawa na asilimia 77.54 ya leng.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema pia kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 Shirika linatarajia kukagua vyama 5000 pia na alisisitiza kuwa kila chama cha Ushirka kiweke kumbukumbu zake sawa ili kuweza kurahisha ukaguzi n ahata rejea pindi zinapohitajika.

Pia amewakaribisha Wananchi na Wadau wote kutembelea katika banda la COASCO lililopo Kijiji cha Ushirika hapa kwenye Uwanja wa Maonesho ya Nanenane 2023 jijini Mbeya kwa ajili kujifunza namna ya uandishi wa vitabu katika vyama vya Ushirika na Ushauri wa kodi zinazohusiana na Vyama vya hivyo.

COASCO ni Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama Vya Ushirika lenye majukumu ya kufanya kaguzi za mahesabu, kusimamia na kushauri vyama vya Ushirika.
Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) CPA Golden Kajaba akitoa huduma katika banda la COASCO kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoaendelea katika viwanja vya John Mwakangale , jijini Mbeya .
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa COASCO kwenye maonesho ya Kimataifa ya kilimo Nane Nane , Jijini Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...