Na Mwandishi wetu Zanzibar
TAASISI ya Bahari ya Dar es Salaam (DMI) imesema imejipanga kikamilifu kutoa taaluma za bahari kwa vijana visiwani hapa ili wanufaike na fursa zilizopo za sera ya uchumi wa buluu.

Kauli hiyo ameitoa jana Muhadhiri wa Chuo hicho Mohamed Kaul Makame katika maonyesho ya nne ya elimu ya juu yaliyofanyika uwanja wa Maisara uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alisema kutokana na kuwa Zanzibar imejikita kwenye kipaumbele cha utekelezaji wa sera ya uchumi wa buluu DMI imeona umuhimu wa kujitokeza visiwani hapa kutangaza taaluma zinazopatikana kwenye chuo hicho.

"Tunashukuru mpaka sasa vijana wengi wa Zanzibar wameonyesha muitikio mkubwa wa kutaka kujiunga na DMI Kwa ajili ya kujipatia taaluma za bahari ili wanufaike kupitia uchumi wa buluu ikiwemo ubaharia na usafirishaji kwa njia ya maji,"alisema Kauli

Katika maelezo yake Makame alisema baada ya vijana hao kupata taaluma hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa sera ya uchumi wa Buluu kwa ufanisi zaidi.

"DMI inaendana na mbadiliko ya teknolojia ambapo tuna mitambo ya kisasa ya kufundishia undeshaji wa meli,mitambo ya uhandisi wa meli na kila baada ya muda tunafanya mabadiliko makubwa ya mitambo hiyo,"alisema

Kwa upande wake Ofisa Udahili wa Taasisi ya Bahari ya Dar es Salaam(DMI), Rehema Athuman Juma alisema chuo hicho kitahakikisha kinajikita zaidi kwenye kutoa taaluma Kwa vijana kupitia fursa zilizopo za sera ya uchumi wa buluu.

Alisema taaluma ya bahari ni nzuri na inatoa fursa kubwa katika sekta ya bahari kama ilivyokuwa imesahaulika kipindi cha nyuma.

" Sasa hivi tunaweza kulima mazao ya baharini ikiwemo kilimo cha mwani pamoja na tukavua samaki kwenye kina kirefu cha maji hivyo DMI inaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Zanzibar ya wamu ya nane kupitia sera ya uchumi wa buluu,"alisema
Muhadhiri wa Chuo hicho Mohamed Kaul Makame akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Nne ya elimu ya Juu , katika Viwanja vya Maisala Zanzibar.
Muhadhiri wa Chuo hicho Mohamed Kaul Makame akizungumza na wananchi waliotembelea banda la DMI maonesho ya Nne  ya Elimu ya Juu Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...