Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma yanapofanyika maonesho ya Wakulima maarufu kama Nane Nane kwa Kanda ya Kati Dodoma. Ushiriki wa Tume katika maonesho hayo ni kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo.
Aidha Tume inapata fursa ya kukutana ana kwa ana na wadau mbalimbali wa Uchaguzi na kuweza kuzungumza nao na kujibu maswali na hoja mbalimbali zinazowakabili. Ufafanuzi kuhusu masuala ya Ucxhaguzi pia unatolewa na maafisa wa Tume waliopo katika banda hilo la Maonesho.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda hilo la kupata ufafanuzi juzi ya mambo yanayowatatizo.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini, Jabir Shekimweri akiwasikiliza maafisa wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakati Mkuu hyyo wa Wilaya alipotembelea banda la Tume katioka Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Kati yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwapa maelezo wanafunzi wa Shule ya Msingi Hijra ya Jijini Dodoma wakati walipotembelea banda la Tume katioka Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Kati yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Wakuu wa Wilaya za Chamwino, Iramba na wenyeviti wa halmashauri za Dodoma leo tarehe 3 Agosti, 2023 wametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye maonesho ya wakulima (Nanenane) Kanda ya Kati yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.
Wananchi mbalimbali wakipata huduma katika Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Wananchi mbalimbali wakipata huduma katika Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...