Kuelekea kilele cha Tamasha la kizimkazi , Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametembelea katika banda la benki ya Equity kushilikiana  na Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF).
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Bi. Isabela Maganga akielezea juu ya mikakati ya benki yetu na ushirikiano  na Taasisi ya MIF kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan hapo jana Zanzibar.  

 

 ***************

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Bi. Isabela Maganga alisema, Kizimkazi na Mkoa wa kusini Unguja kwa ujumla ni sehemu ya utekelezaji wetu wa dhamira ya benki ambapo inalenga kubadilisha maisha ya wananchi kiuchumi na kijamii kwa kuwawezesha vijana ,wanawake, na wajasiliamali wadogo na wakubwa kwa kushilikiana na Taasisi ya MIF.

Aliendelea kusema “Ushirikiano wa benki ya Equity na Taasisi ya MIF umelenga kuleta maendeleo hapa Zanzibar kwa watoto wa kike na vijana kwa ujumla, ikiwa lengo kwa upande wa vijana ni kuwaongezea ujuzi kupitia VETA ikiwa ni kusaidia katika suala zima la nishati na mazingira kwa kuhakikisha kaya zinapata nishati safi za kupikia ili kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuwaepusha na magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya nishati chafu kama kuni na mkaa, kuhakikisha vijana wanashiriki kwenye upandaji miti na kulinda vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi”.

“lengo pia ni kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo wakike haswa ya kifedha na jinsi ya kuendesha biashara zao ili ziweze kukua na kutengeneza faida itakayosaidia kuendesha maisha yao. Pamoja na hayo, tutaingia makubaliano ya dhamana wezeshi kusaidia kupunguza hatari ya mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. Wengi wamekuwa wakishindwa kulipa mikopo yao sio kwa sababu biashara mbaya bali ni kukosa elimu ya kifedha”, Alisema Bi. Isabela

 


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...