Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji kinaendelea na Operesheni maalum iliyoanza Julai 19, 2023  na inayoendelea katika kudhibiti uhalifu ukanda wa Bahari ya Hindi.

Aidha katika Operesheni hiyo Kikosi kazi cha Operesheni cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam wakitumia boti ya Polisi walikamata mitumbwi miwili isiyokuwa na jina wala usajili huko maeneo ya feri Wilaya ya Ilala, na Tafico Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam, iliyokuwa inatumika kuvua samaki kwa kutumia nyavu haramu aina ya kokoro.

Katika hatua nyingine, operesheni hiyo Julai 25, 2023 majira ya saa nane usiku huko maeneo ya Kunduchi katika bahari ya hindi askari Polisi kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wakiwa doria walifanikiwa  kuwakamata Abdalla Jecha @ omary (37) na Khatibu Kombo (23) wakiwa  na Jahazi liitwalo SAFINIA lisilokuwa na namba za usajili likiwa limebeba mafuta ya kupikia aina ya ACTER dumu 364 na kila moja likiwa na lita 20 yakitokea Unguja kwenda Dar es Salaam kwa kupitia bandari bubu ya kunduchi wakiwa na nia ya kukwepa ushuru wa forodha.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini watuhumiwa hao hawakuwa na nyaraka zinazothibitisha uhalali wa umiliki wa mizigo hiyo ya mafuta ya kupikia pamoja na nyaraka za usafirishaji. Jeshi la Polisi linawahoji watuhumiwa hao kwa kina na baadae taratibu nyingine za sheria ziweze kuchukuliwa.

Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara nyingine za serikali kuhakiki mzigo huo, pia  linawapongeza wananchi wote ambao wanachukia uhalifu wa aina zote na ambao wanatoa taarifa zinazo pelekea kubaini na kuzui uhalifu.

Hata hivyo Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa wafanyabiashara wasio na uadilifu kuacha kusafirishaji mizigo kwa njia ya bahari bila kuwa na nyaraka za mizigo hiyo, Jeshi la polisi Kikosi cha Wanamaji  halitasita kuwakamata na kufikisha kwenye vyombo vya sheria na hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...