Njombe

Baadhi ya wanaume wa kata ya Kitandililo halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamepaza sauti zao na kuomba kusaidiwa kutokana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa kutoka kwa wake zao ikiwemo vipigo pamoja na kuvutwa sehemu za siri (uume) pindi wanapokosea.

Wanaume wameweka wazi katika mkutano wa mbunge wa jimbo hilo Deo Sanga (Jah People) katika kijiji cha Ibatu ambapo wamesema baadhi yao wamekuwa wakifanyiwa ukatili huo kutokana na ukali wa wake zao huku wengine wakijipangia muda wanaotaka kurudi nyumbani.

"Wanaume tunanyaswa sana, na wamama wengine wamekuwa wababe ukiwaambia wawahi kurudi wao wanarudi mpaka saa nne au saa tano wengine muda wanao rudi haueleweki"wamesema baadhi ya wanaume.

Stella uhemba ni diwani wa viti maalum katika halmashauri hiyo amekiri kupokea malalamiko hayo awali kutoka kwa badhi ya wanaume ambapo amesema wanawake wamekuwa wakiwategea na kuwavuta sehemu za siri ambapo umekuwa mtindo wa wanawake wa kata hiyo huku diwani wa kata ya Kitandililo Imani Fute akibainisha kuwa wameanza kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili.

Mbunge wa jimbo hilo Deo Sanga amekemea vitendo hivyo na kuwataka wanawake kutambua nafasi za waume zao katika familia "Na vitabu vitakatifu vinakataa akina mama punguzeni ukali,kwenye nyumba mwenyekiti ni baba,katibu ni mama na watoto ni wajumbe sasa mama unataka uwe mwenyekiti a a mpungeze ukali"


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...