Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
Katika kuhakikisha afya ya mwanadamu inaimarika na kuwa salama, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma imeendelea kutoa tiba, kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, kutoa elimu ya vitendo Kwa wanafunzi na watarajali wa mbalimbali.
Kwa upande wa tiba hospitali hiyo ina madakitari bingwa wa upasuaji, mifupa, uzazi kwa kina mama na mtoto, meno, macho, pua, koo, na sikio, magonjwa ya ndani, ngozi na magongwa ya zinaa.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt Ernest Ebenzi ameyabainisha hayo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma kuelezea kuhusu utekelezaji na vipaumbele vya hospitali hiyo kwa mwaka 2023/2024.
Dkt Ebenzi amesema hospitali hiyo kwa siku inapokea wagonjwa zaidi ya 1,500 na ina uwezo wa kulaza wagongwa 250 hadi 350 Kwa wakati mmoja.
"Kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 idara ya magongwa ya nje na dharura ilihudumia wagonjwa 251,174 wagonjwa 13,607 walikuja Kwa utaratibu wa rufaa, 120,263 (48%) walitibiwa kwa bima ya NHIF, 8,174 (3%) walikuwa na bima nyingine.16,896 (7%) walikuwa wa CHF, na 105,841(42%) walipata huduma kwa njia nyingine za uchangiaji ikiwemo wa msamaha. Aidha wagonjwa 32,090 walilazwa.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja yaani 2022/2023 Hospitali ilifanikiwa kufanya Kliniki tembezi katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Dodoma ambapo wagonjwa 552 walihudumiwa.
Wastani wa mahitaji ya damu kwa mwaka katika Hospitali ya Rufaa ya Dododma ni chupa/units 5,400, kipindi cha mwaka 2022/2023 chupa/Units 5,368 zilikusanywa sawa na asilimia 99% na, hakuna mteja aliyekosa damu.
Katika Kitengo cha uchunguzi kwa njia ya mionzi (Radiolojia) kwa mwaka 2022/2023 kilifanikiwa kufanya jumla ya vipimo 37,975 vya aina mbalimbali.
Hospitali imefanikiwa kununua vifaa tiba vya kisasa ikiwemo; CT- Scan, X- Ray mashine 3 za kisasa zaidi kutoka mashine 1, mashine za Ultrasound 4, mashine za kisasa za maabara na vitendanishi, tunafanya vipimo 136 vinavyosaidia wananchi kutambua changamoto mbalimbali za afya zao.
Dkt Ebenzi amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanya mabadiliko makubwa katika uboreshaji wa jengo ya dharura katika hospitali hiyo ambapo wagonjwa 34 wanapata huduma za uchunguzi, vipimo na malipo ya huduma kwa wakati mmoja na uharaka zaidi kulinganisha na hapo awali wagonjwa wanne tu.
Aidha Dkt Ebenzi ametaja
Vipaumbele vya Hospitali hiyo kwa Mwaka 2023/2024 imetengewa Shilingi bilioni 24, huku hospitali hiyo itaendelea kuwahudumia wananchi kwa wakati na huduma bora kwa gharama ndogo, kutumia muda mfupi katika kumuhudumia mgonjwa pamoja na uhakika wa dawa za kutosha.
Hata hivyo Hospitali inaendelea kukarabati na kujenga majengo kwa ajili ya kutolea huduma mbalimbali za afya, kuendelea kupiga hatua katika kutoa huduma bora kwa kuzingatia sayansi na teknolojia ya kisasa , kufanya tafiti mbalimbali, kuwasomesha watumishi wa hospitali, Kujenga jengo la gorofa 5 kwa ajili ya sehemu mbalimbali za kutolea matibabu, Kuboresha mikakati ya ukusanyaji damu pamoja na Kuendelea kuboresha na kujenga miundombinu ya hospitali kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...