Kampuni ya simu za mkononi yenye makao makuu yake nchini Hong Kong yaendelea kupasua anga kimataifa hii ni kufuatia ushindi wa Tuzo ya usanifu ya muundo wa bidhaa/vyombo vya habari na electroniki ya nyumbani kwa Mwaka huu wa 2023.

Infinix imejipatia Tuzo hiyo kupitia Infinix NOTE 30, muundo wa simu hii umeipa heshima kubwa kampuni hiyo katika Tuzo hizii za Usanifu wa Ndani, Usanifu wa Mandhari, Usanifu wa Picha na Muundo wa Bidhaa ambao hutunukia wabunifu bora zaidi duniani kote kila Mwaka. https://dna.paris/winner/zoom.php?eid=71-90434-23)

“Hii ni heshima kubwa kwetu kama kampuni ambayo inakuwa kwa kasi kubwa inayotokana na uzalishaji wa bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa gharama nafuu,” imeeleza kampuni hiyo”.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo inanufaika vyema na bidhaa za kampuni hiyo, imekuwa na mchango mkubwa katika kufanya teknolojia ya mawasiliano kupitia njia ya simu kuenea kwa wepesi.
Hii siyo mara ya kwanza kwa kampuni hii kushinda tuzo hizo za kimataifa mwaka 2021 pia ilitwaa tuzo ya bidhaa yenye nidhamu Infinix ZERO 8 katika kitengo cha mawasiliano huko barani Asia.
Tutegemee makubwa kutoka kwao kasi yao katika uzalishaji wa simu zenye teknolojia ya hali ya juu si yakubeza, Infinix si hodari tu kwenye designing wako vyema pia na teknolojia ya fast chaji na wireless chaji. NOTE 30 VIP ina fast chaji ya WATT 68 na wireless chaji ya WATT 50 pamoja na kureverse chaji ni simu inayofanya vyema kwa sasa duniani kote.

Hongera nyingi sana kwa ushindi huu na katika kukuza teknolojia ya mawasiliano kupitia njia ya simu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...