Na Rahma Khamis Maelezo                 28/8/2023

 

Mkuu wa Wilaya ya kaskazini “B” Hamid Seif Said  ameitaka jamii kutambua na kuthamini mchango  unaotolewa na walimu wa Madrasa katika kuwapatia maelezi  bora watoto wao.

 

Akizungumza na wazazi ,walimu na wanafunzi wa Madrasa za Shehia   ya Kiwengwa Kumbaurembo  katika Bonaza la mashairi ya papo kwa papo amesema walimu hao wamekuwa na kazi ngumu yakujitolea.

 

 Amesema waalimu wa Madrasa wanajitahidi katika kuwafundisha watoto malezi mema  kwani muda mwingi watoto hao wanakuwepo chini ya  uangalizi wao hivyo ni vyema kuthamini mchango wanaoutoa bila ya malipo.

 

“Waalimu  wanatumia nguvu nyingi kusimamia vizuri  malezi ya watoto wetu, kwani tunapowawezesha na kuthamini michango yao wataongeza ari na kasi ya kufundisha  na kuwafanya  kuwa watoto wema na bora katika jamii”alisema Mkuu wa Wilaya.

 

Aidha amesema kuwa wazazi wamekuwa wakitumia gharama kubwa kuwapeleka watoto Skuli na kusahau thamani na mchango wa waalimu wa Madrasa kwa watoto wao jambo ambalo linarejesha nyuma maenedleeo ya walimu hao .

 

Ameongeza kuwa  waalimu  wanatumia muda mwingi kubaki na watoto  Madrasa  jambo linalopelekea kukosa  nafasi ya  kujitafutia baadhi ya mahitaji ya lazima hivyo ipo haja ya kuwawezesha walimu hao kuweza kujikimu katika mahitaji yao.

 

“ Ongezeko la madawa ya kulevya na Udhalilishaji linachangiwa na ukosefu wa  malezi bora  ya watoto wetu ,ambao unachangiwa na kutokuwathamini walimu wa madrasa hivyo tushirikiane na walimu hao katika malezi ili  kuondoa changamoto hizo  ” ,alisema.

 

Aidha Mkuu huyo aliwasisitiza wazazi kukaa na watoto wao kiurafiki  zaidi ili kuwapa  fursa ya kutoa taarifa za udhalilishaji  pindi wanapo kumbana nazo.

 

Akizungumzia suala la wasanii amefahamisha kuwa  watunzi  wa mashairi ni wasanii kama wasanii wengine  kwani  wanaelimisha jamii juu ya mambo mbali mbali ikiwemo athari za matumizi ya   madawa ya kulevya,maradhi yasioambukiza  na malezi ya watoto.

                              

Akitoa maelezo mafupi kuhusu Bonanza la Mashairi hilo Katibu wa Chama cha Kuendeleza Washairi (CHAKUWAZA) Maimuna Hashim

  amesema lengo la Bonaza hilo   ni kuihamasisha jamii kuatambua thamani ya walimu wa madrasa,pamoja na kutoa elimu juu ya athari za matumizi ya  dawa za kulevya na maradhi yasioambukiza kupitia  Sanaa za mashairi.

 

Katibu ameeleza kuwa chama cha kuendeleza washairi kinafanya kazi kwa kujitolea na  kimefanikiwa  kutoa elimu kwa jamii,kupitia  mashairi, kukuza lugha ya Kiswahili na kuendeleza utamaduni.

 

Alifahamisha kuwa  Bonanza Hilo ni la Tatu Kufanyika kwa mwaka huu  ambapo Bonaza la kwanza lilifanyika Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja likiwa na lengo la kuhamasisha jamii juu ya kupinga vitendo vya udhalulishaji.

 

Aidha ameiomba jamii kufika chama cha washairi kupata washairi waliosajiliwa kuweza kutumia sanaa zao  katika shughuli mbalimbali wanazozifanya.

 

Nao wazazi na walezi wa watoto hao wameahidi kuongeza umoja na  ushirikiano kwa waalimu wa Madrasa ili    kuzidisha malezi bora ya watoto wao kwani  kufanikiwa katika malezi kutasaidia kuondoa vitendo vya udhalilishaji.

  

Jumla ya shilingi laki tano za Kitanzania zilipatikana kwa ajili ya walimu wa Madrsa za Kiwengwa Kumbaurembo katika Harambee  iliyofanyika kwenye Bonaza hilo .

 

 

 Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Hamid Seif Said akizungumza na,Wazazi na Wasanii wa mashairi kuhusiana na thamani ya Walimu wa Madrasa wakati wa Bonaza la mashairi ya papo kwa papo lililofanyika Viwanja vya Skuli ya Kiwengwa Kumbaurembo.

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Hamid Seif Said akisikiliza maelezo kutoka kwa msanii wa Mashairi Kassim Yussuf (zero kasorobo) wakati alipofika Viwanja vya Skuli ya Kiwengwa Kumbaurembo kushiriki Bonaza la Mashairi  ya Papo kwa papo.

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Hamid Seif Said akizungumza na,Wazazi na Wasanii wa mashairi kuhusiana na thamani ya Walimu wa Madrasa wakati wa Bonaza la mashairi ya papo kwa papo lililofanyika Viwanja vya Skuli ya Kiwengwa Kumbaurembo.
Wasanii wa Mashairi Kassim Yussuf (zero kasorobo) na Issa Ali (Daktari wa mashairi) wakitoa burudani ya Ushairi wenye maudhui ya kutambua thamani ya Mwalimu wa Madrasa wakati wa Bonaza la Mashairi ya Papo kwa papo lilifanyika Viwanja vya Skuli ya Kiwengwa Kumbaurembo.
-Wasanii wa Mashairi kutoka Chama cha Kuwaendeleza Washairi Zanzibar  CHAKUWAZA  wakisoma utenzi wenye maudhui ya kutambua thamani ya Mwalimu wa Madrasa wakati wa Bonaza la Mashairio ya Papo kwa papo lilifanyika Viwanja vya Skuli ya Kiwengwa Kumbaurembo.

Wasanii wa Mashairi kutoka Chama cha Kuwaendeleza Washairi Zanzibar  CHAKUWAZA  wakisoma utenzi wenye maudhui ya kutambua thamani ya Mwalimu wa Madrasa wakati wa Bonaza la Mashairio ya Papo kwa papo lilifanyika Viwanja vya Skuli ya Kiwengwa Kumbaurembo.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBARMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...