Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wa wilaya hiyo huku akitumia nafasi hiyo kueleza fedha ambazo Rais amewapatia mwaka jana Sh.bilioni 152 na kati hizo Sh.bilioni 43.7 zilitumika kujenga barabara.

Matinyi ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Mbagala Zakhiem na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Mkuu wa Mkoa tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan, fedha ambazo amtupatia katika mwaka wa fedha ulioisha Juni mwaka huu zimetuwezesha kufanya mambo makubwa ya maendeleo.Rais alitupatia Sh.bilioni 152 na kati ya hizo fedha tumezitumia kujenga barabara.

“Mkuu wetu wa Mkoa leo umejionea mwenyewe katika kila mtaa tuliokuwa tunakatiza ni lami kama sio lami ni zege .Lakini mbali ya ujenzi wa miundombinu ya barabara Sh.bilioni 61.6 zilitumika katika miradi ya umeme katika wilaya yetu tunayo wilaya kubwa hasa kwa idadi ya watu, eneo linaweza lisiwe kubwa baada ya kumega eneo la kuwasaidia ndugu zetu wa Kigamboni

“Wilaya ya Temeke inakaribia watu milioni 1.4 sasa huduma za jamii zinahitaji fedha nyingi na ndio maana Rais wetu amekuwa akitupatia fedha hizo. Upande wa maji kwa mwaka wa fedha uliopita zimetumika Sh.bilioni 15.5 na kwasababu tuna watoto wengi Rais alitupatia Sh.bilioni 7.6 zilizotusaidia kwenye upande wa elimu ya msingi tu ambapo shule sita madarasa 147 , matundu ya vyoo ,madawati na vifaa mbalimbali tumefafanikisha kupitia fedha hizo,”amesema Matinyi.

Aidha amesema katika shule za sekondari, wilaya hiyo kiwango cha ufaulu kitoka shule za msingi kwenda sekondari kiko juu ya asilimia 95 , hivyo wana mahitaji makubwa ya shule za sekondari lakini Rais Samia aliwapatia Sh.bilioni 10.

Pia ameeleza kwenye upande wa afya Rais aliwapatia Sh.bilioni 6.1 na hizo hazijumuishi ambazo alivyoona Mkuu wa mkoa wakitembelea hospitali.”Hii inaonesha Rais anavyowajali wananchi wa Temeke, tunakuomba fikisha shukrani zetu kwa Rais na tunamhakikisha kila senti inayokuja Temeke itatumika kama alivyokusudia.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...