Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, leo imetembele Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa, pamoja na kupokea taarifa ya Maendeleo ya Chuo Hicho.

Kamati hiyo ilipokelewa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar J. Kipanga na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Rwekaza Mukandara, ambao kwa pamoja walitembelea miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ukiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la hospitali kwa ajili ya vipimo vya mionzi, kwa lengo la kuboresha huduma za kitabibu katika hospitali ya Chuo hicho.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha ziara ya kukagua miradi, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezi, Mhe. Husna Juma Sekiboko, amepongeza jitihada kubwa za uongozi wa Chuo katika kuanzisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa makusanyo ya fedha za ndani na kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Elimu, kuangali namna bora ya kuongezea nguvu miradi hiyo ili kukamilika kwa wakati.

“ Kwa hakika huu ni uzalendo mkubwa kwa Taifa, tumetembelea na kuona uwekezaji mkubwa wa jengo la hospitali kwa ajili ya vipimo vya mionzi, na ujenzi wa uzio katika eneo la nyumba 29 zilizonunuliwa na Chuo kwa ajili ya Watumishi, kwakweli miradi hii ikikamilika itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi hususani wakazi wa Dodoma, na wanafunzi ambao wanasomea masomo ya Afya, kutumia Hospitali ya hiyo kufanya majaribio kwa vitendo” alisisitiza

Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omar J. Kipanga, ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea UDOM, na kuahidi Wizara kwa kushirikiana na wadau wenigne muhimu katika Sekta ya Maji kuendelea kufuatilia na kushughulikia changamoto ya maji iliyoanishwa kwa Kamati wakati wa ziara hiyo.

“ Ni kuahidi Mwenyekiti, suala la maji kwa Chuo chetu nila kipaumbele, na tayari kama Wizara tulishaweka mikakati ya kushughulikia changamoto hiyo kwa kushirikisha Wizara ya Maji’ alisema

Akiwasilisha taarifa ya Chuo kwa Kamati, Makamu Mkuu wa Chuo Pof. Lughano Kusiluka amesema, ujenzi wa Jengo la Huduma za mionzi katika Hopsitali ya Chuo umegharimu Tshs. Bilioni 3.4 na tayari umekamilika kwa asilimia 98, na hatua inayoendelea sasa ni kufunga umeme pamoja na kuanza mchakato wa manunuzi ya vifaa na uwekaji Samani. 

Aidha ameeleza ununuzi wa nyumba za watumishi umegharimu Tshs. Bilioni 2.2; huku gharama za ujenzi wa uzio zikiwa ni Tshs. kwa Milioni 179. Fedha zote zimetokana na vyanzo vya ndani, na kwamba Menejimenti inaendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza wigo wa kukusanya mapato yatakayosaidia utekelezaji wa shughuli nyingine za maendeleo chuoni hapo kama zilivyoanishwa katika Mpango Mkakati wa Chuo.

Kamati hiyo imehitimisha ziara yake kwa kusisitiza UDOM kuendelea kuboresha eneo la Taaluma, kwa kubuni program zinazoendana na mahitaji halisi ya soko, pamoja na kukazia nidhamu kwa wanafunzi ili kuendeleza sifa nzuri ya kuwa Chuo Bora nchini Tanzania na Afrika. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, akizungumza wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara Chuo Kikuu Cha Dodoma leo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omar J. Kipanga, akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo walipotembelea UDOM. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Husna Juma Sekiboko na kushoto ni Dkt. Edward Hosea, akimwakilisha Katibu Mkuu MoEST.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakipokea maelezo kwa mtaalamu wa ujenzi wa jengo la hospitali kwa ajili ya vipimo vya mionzi linaloendelea kujengwa chuoni hapo.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ikikagua ujenzi wa uzio  katika eneo lenye nyumba 29 za watumishi. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Rwekaza Mukandala (mwenye suti nyeusi), akiwa ameambatana na Mhe.  Dkt. Tea Ntala, katikati ni Prof. Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Husna Juma Sekiboko.

Kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Elimu, Utamaduni na Michezo kikiendelea katika ukumbi wa Senate wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Kikao hicho kilihusisha wajumbe wa Kamati, Uongozi na Menejimenti ya Chuo.

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, baada ya kuhitimisha ziara yao chuoni hapo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...