Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la saba la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ambalo litafanyika Jijini Dodoma tarehe 29, mwezi ujao (Septemba).

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa amewaambia waandishi wa habari Jijini hapa jana kuwa kongamano hilo  umuhimu litatanguliwa na wiki ya uwezeshaji sambamba na maonesho ya siku tatu ya wajasiriamali yatakayoanza septemba 26 hadi 28 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

 

“Maenesho hayo ya siku tatu kabla ya kongamano yana maana kubwa katika dhana nzima ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwani wajasiriamali watapata fursa ya kipekee kuonyesha biashara zao kwa watanzania na jinsi wanavyopata mafanikio kupitia uwezeshaji,” alisema Bi. Issa.

 

Kwa mujibu wa Katibu huyo Mtendaji wa Baraza, Kauli Mbiu ya Kongamano hilo la saba ni ‘Uwezeshaji kwa Uchumi Endelevu’ kwani inatoa fursa ya kujadili kwa kina masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa uchumi endelevu wa Tanzania.

 

“Kongamano litatoa pia fursa ya kutathmini utekelezaji wa sera ya uwezeshaji pamoja na taarifa mbalimbali ya utekelezaji wa mambo yaliyokuwa kwenye kongamano la sita ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaagiza wakuu wa mikoa yote kuanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi,” alisema.

              

Bi.Issa alisema wakati wa kongamano, tuzo pia zitatolewa kwa wote waliofanya vizuri ikiwemo mkoa uliofanya vizuri, wajasiriamali na taasisi  mbalimbali za uwezeshaji  kwani mafanikio mengi yameshapatikana chini ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

“Kama Baraza tunamshuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo na ufuatiliaji wake wa kutaka  kuona kuwa watanzania wengi na hasa wanawake na vijana wananufaika zaidi na uwezeshaji sambamba kuinua vipato vyao na kuchangia pato la taifa,” alisema.

Alisema kongamano litahusisha  Wizara, Mashirika, Wakala na Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi chini ya mwamvuli wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Mikoa, Halmashauri, Wajasiriamali, Taasisi za Fedha, Taasisi za Elimu, Tafiti, Wawekezaji pamoja na wadau wengine wa masuala ya uwezeshaji.

“Wananchi wote wanakaribishwa wanakaribishwa kujionea na kujifunza masuala mazima ya uwezeshaji, upatikanaji wa mitaji, fursa zilizopo kwenye miradi ya mkakati,masoko na hata kutengeneza mtandao wa watu, Taasisi au Kampuni ya kujiendeleza kiuchumi,” alisisitiza Bi. Issa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Huduma wa Baraza, Bw. Gwakisa Bapala (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi  wa Uwezashaji na Ushiriki wa watanzania kwenye Miradi ya Kimkakati, Bw.Silaji Nalikame muda mfupi baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi litakalofanyika septemba 29, mwezi ujao jijini hapa jana. Picha na Mpiga Picha Wetu)

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habarikuhusu Kongamano la Saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi litakalofanyika septemba 29, mwezi ujao jijini hapa jana..Wengine ni  Mkurugenzi wa Huduma wa Baraza, Bw. Gwakisa Bapala (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi  wa Uwezashaji na Ushiriki wa watanzania kwenye Miradi ya Kimkakati, Bw.Silaji Nalikame . Picha na Mpiga Picha Wetu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...