Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi amesema zao la Mwani ni zao linaloelekea kushika kasi kubwa katika soko la Dunia wakati Zanzibar inashika nafasi ya kwanza katika kuzalisha zao hilo.

Ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa vifaa bora vya kuanikia Mwani ambavyo ni vichanja vya kisasa 220 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 289 kwa wakulima iliyofanyika Bweleo , Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Mama Mariam Mwinyi amesema zao la Mwani ni dhahabu ya Zanzibar kwani unaleta tija ya kiuchumi na pia kwa mwili wa binadamu kwani Mwani ni chakula na una virutubisho vingi sana ikiwemo madini ya chuma ambayo yanaweza kutumika na kina mama wajawazito, Mwani pia hutumika kama mbolea kwa mazao mengine na vipodozi.

Vilevile, amesema ukiachana na Bara la Asia ambao wanaongoza kidunia.Zanzibar inashika hatamu kwa kulima Mwani Afrika.

ZMBF imekuwa mstari wa mbele kukuza zao la Mwani kupitia lengo lake la kimkakati namba moja la kuwawezesha Wanawake na Vijana kiuchumi kupitia ukulima wa Mwani.

Amewashukuru Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kushirikiana katika upatikanaji wa vifaa bora vya kuanikia Mwani ambavyo vitaongeza mnyororo wa thamani kwa zao la mwani Zanzibar.

đź—“️19 Agosti, 2023

đź“ŤBweleo, Wilaya ya Magharibi B , Mkoa wa Mjini Magharibi.












 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...