Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamefurika katika banda la kampuni ya Lake Gesi lililopo katika viwanja vya nanenane mkoani humo kununua majiko na mitungi ya gesi inayouzwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati vijijini(REA) kwa Bei ya Punguzi katika viwanja vya Maoneesho hayo ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Akizungumza katika viwanja hivyo Menena Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group,Matina Nkurlu alisema wao kama kampuni wamekuja na kampeni mpya ya"Pika na Pakua na Lake gesi" ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Kampeni ya Rais,Mama Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanamshusha Mama kuni kichwani na kuhakikisha matumizi ya Gesi kwa kupikia yanaenea nchi mzima.
Katika kuhakikisha hilo Lake Energies kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati vijijini(REA) Tunahakikisha tunawafikia wanawake nchi nzima na kwa sasa tumeanzia mkoa wa Mbeya napenda tu kuwahakikishia wakazi wa mkoa huu kuwa tuna mzigo wakutosha na kama unavyoshuhudia alisisitiza Nkurlu.
Nae mmoja wa kinamama anayejishughulisha na Biashara ya Mama Lishe, Atupelile Mwakakasita alisema wanaishukuru serikali kupitia REA na kampuni ya Lake Energies kwa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kwa kuwaletea promosheni hii ya kuuza mitungi midogo kwa gharama nafuu.
Maonesho ya Nanenane yalifunguliwa tarehe Moja mwezi huu na Makamo wa Rais, Dkt Isdori Mipango yanayotarajiwa kufungwa tarehe 10 mwezi huu.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mkata(wapili kushoto) akipokea mtungi wa gesi toka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group, Matina Nkurlu(Kulia)baada ya kuununua katika banda hilo lililopo katika viwanja vya nanenane mkoani Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...