Baadhi ya Wananchi wakipata elimu ya bima ya kilimo katika banda la NIC Insurance kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale jijiji Mbeya.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
NIC Insurance linawahamasisha wananchi kutembelea maonesho ya Nane Nane Kitaifa Kanda ya Mbeya kupata elimu ya huduma ya bima kilimo katika maonesho hayo.
Katika kupata elimu bima hiyo pia wananchi wanaweza kukata bima mbalimbali na kupata ndani ya muda mfupi kutokana na mifumo iliyowekwa.
Akizungumza na Michuzi Blog ndani ya Maonesho ya Kilimo Kitaifa Kanda Mbeya Nane Nane Meneja wa NIC Kanda ya Mbeya Justine Iseni amesema wamejipanga kutoa huduma ndani ya maonesho hayo.
Amesema NIC Insurace imeanza kutoa bima katika mazao mbalimbali kutokana majanga wanayopata katika sekta hiyo kuwafuta machozi .
Iseni amesema kuwa huduma zote za bima zimesogezwa katika Maonesho ya Nane Nane ili wananchi wapate bima mbalimbali zitazowasaidia kwenye majanga hata katika biashara.
Amesema NIC imejipanga kuwafikia wadau wote wakiwemo wakulima na wafugaji kupata bima ambapo kilio cha wananchi kitakuwa kimeisha.
Amesema kuwa NIC imekuwa na mifumo ya tehama rahisi na kufanya mtu kujisajili na kuweza kupata bima moja kwa moja.
Aidha amesema kazi inaendelea lakini kazi hizo lazima tuliochini tuhakikishe tunatoa huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...