Na Nasra Ismail, Geita
MBUNGE wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu amesema Hospital ya Halmashauri ya Mji wa Geita inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa dawa.
Kanyasu ameyasema hayo baada ya kutembelea hospitali hiyo na akiwa hapo alipokea uwepo wa changamoto mbalimbali katika hospitali hiyo, hivyo ameomba hatua za haraka zichukuliwe kuondoa changamoto zilizopo kwa lengo la kuboresha utoaji huduma za afya ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Akifafanua zaidi pia katika hospitali hiyo kuna changamoto ya idadi ndogo ya watumishi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma za matibabu ambapo ameeleza kwa siku hospitali hiyo wanapokea wagonjwa 300.
"Kutokana na changamoto zilizopo tunaiomba Serikali lazima itafute utatuzi haraka, haipendezi kuona au kusikia hospitali yetu ya Halmashauri ya Mji wa Geita inakabiliwa na uhaba wa dawa.Mwito wangu kwa Serikali ni vema ikahakikisha inasimamia huduma zinazotolewa kama ilivyoahidi, " amesema Mbunge Kanyasu.
Awali Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Sunday Aron amesema hospital hiyo ina jumla ya watumishi 122, hivyo bado kuna uhitaji wa watumishi wengine ili kukidhi mahitaji ya hospital hiyo.
"Tukiongezewa watumishi 320 angalau tutakuwa na watumishi ambao wanaweza kuwa na uwiano wa kuhudumia wagonjwa.Tumeendelea kuimarisha na kuboresha maeneo ya kutolea huduma za dharula na wagonjwa wa nje. Pia huduma za kinywa, meno pamoja na macho, " amesema Aron.
Kwa upande wake Ofisa Tabibu katika hospitali hiyo Mohammed Jembe amemuomba Mbunge Kanyasu kuwawezesha kupata gari ya wagonjwa kwani imekuwa ikiwalazimu kuazima gari hospitali ya Nyankumbu.
"Kuomba gari la wagonjwa katika Hospitali ga Nyankumbu kuna mlolongo mrefu, hivyo wakati mwingine inatulazimukusafirisha wagonjwa waliopata rufaa kwa usafiri wa bajaji."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...