NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wametakiwa kuhakikisha wanawaunganishia huduma ya majisafi wanufaika wa Mradi wa maji wa Chalinze awamu ya tatu kwa mkopo baada ya kukamilika kwa mradi huo ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa haraka na kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Wito huo umetolewa leo Agosti 28,2023 na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami ambayo ni moja ya shughuli zilizofanyika kwenye utekelezaji wa mradi huu.

"Nitoe maagizo kwa DAWASA, muwaonganishie huduma ya majisafi wanufaika wa mradi huu kwa mkopo kwa kuzingatia masharti nafuu na vigezo rafiki ili kila mwananchi apate huduma ya majisafi karibu na makazi yake". Amesema

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mhandisi Maryprisca amesema serikali itaendelea kuhakikisha inawasogezea wananchi huduma ya majisafi kwa ukaribu ili kuondokana na kadhia ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Pamoja na hayo Naibu Waziri Maryprisca amewapongeza watendaji wa DAWASA kwa kuhakikisha kazi ya utekelezaji wa mradi huo ni nzuri ambao unakwenda kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okashi ameipongeza Wizara ya Maji kwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya ya Bagamoyo hususani mradi wa maji wa Chalinze awamu ya tatu ambao umeenda kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji iliyokuwepo kwa mda mrefu.

"Tutakuwa wachoyo wa fadhila kama tutaacha kumshukuru Rais wetu msikivu ambaye kwa namna kubwa ametusaidia wanawake wa Wilaya ya Bagamoyo sasa upatikanaji ni wa uhakika, pia tunawapongeza DAWASA kwa kuendelea kuipa ushirikiano ofisi yangu ambao tumezunguka nao kwenye kata zote 26 kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa wilaya ya Bagamoyo" amesema Mhe. Okashi

Nae Mwakilishi wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Shabani Mkwanywe amesema mradi wa maji wa Chalinze ni moja ya miradi ya mfano ya vijijini kutokana na usanifu mzuri uliofanyika na utaenda kunufaisha takribani vijiji 59 vya Pwani, Morogoro vijijini na Wilaya ya Handeni Tanga.

"Mradi wa maji wa Chalinze awamu ya tatu umehusisha upanuzi wa mtambo wa kuzalisha maji Wami, ulazaji wa bomba za inchi 12 na 16 kwa umbali wa kilomita 24, ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji ya chini na juu takribani 19 na ujenzi wa vizimba vya kuchotea maji takribani 351 na umegharimu zaidi ya bilioni 44 na unategemea kunufaisha wakazi zaidi ya 200,000" ameeleza Mhandisi Mkwanywe.

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okashi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo wakati Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.

Mwakilishi wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Shabani Mkwanywe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo wakati Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (hayupo pichani) alipokuwa anazungumza wakati wa ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akimtua ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akitazama baadhi ya mitambo ya ukusanyaji maji Wami wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akiongozana na baadhi ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okashi pamoja na Mwakilishi wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Shabani Mkwanywe wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akimsikiliza mmoja wa viongozi wa DAWASA wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.


Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akisaini kitabu cha wageni wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua upanuzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Wami leo Agosti 28,2023 mkoani Pwani.


PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...