Na Humphrey Shao,Michuzi TV
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imekamilisha Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme kilichopo Ifakara Kinachotajwa kwenda kuleta neema ya umeme wa uhakika kwa wananchi wa wilaya za Kilombero na Ulanga mkoani Morogoro, ambao walikuwa na changamoto ya kupata umeme mdogo na wenye kukatika mara kwa mara.
Akizungumza na Michuzi TV Meneja wa Mradi kutoka REA, Mhandisi Romanus Lwena amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho ambao umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Tanzania utakuwa mwarobaini wa kukatika katika kwa umeme katika Wilaya ya Kilombero na Wilaya za jirani.
" azma ya kutekeleza Mradi huu ilifikiwa baada ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA )kubaini changamoto ya umeme mdogo waliyokuwa wakiipata wananchi wa maeneo hayo na hivyo kudhamiria kuitatua" Amesema Rwena.
Aidha Mradi wa ujenzi wa Kituo hicho chenye uwezo wa MVA 20 wa Msongo wa Kilovoti 220, kumetokana na mikakati thabiti wa Serikali kupitia REA, inayolenga kuhakikisha wananchi wote wakiwemo waishio vijijini wanapatiwa umeme wa uhakika.
Alimaliza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DR. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha za ujenzi wa kituo hicho ambacho ni Mkombozi kwa wananchi.
Meneja Mradi wa Wakala wa umeme Vijijini Rea, Mhandisi Romanus Lwena, akizungumza na Waandishi wa habari katika kituo cha kupoza Umeme Ifakara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...