Na Muhidin Amri,Mbambabay

SERIKALI imetenga shilingi bilioni 22 zitakazotumika kujenga daraja la Mitomoni katika mto Ruvuma linalounganisha wilaya ya Nyasa na Songea mkoani Ruvuma.

Haya yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Gofrey Kasekenya wakati akizungumza na wananchi wa Mji wa Mbambabay wilayani Nyasa.

Amesema, tayari serikali imelisanifu daraja la mitomoni na Mkandarasi ameshapatikana na kwamba ujenzi wa daraja hilo unatarajia kuanza mwaka huu wa fedha.

Amesema, kutokana na umuhimu wa barabara ya Nangombo hadi Chiwindi mwambao mwa ziwa Nyasa,serikali imeingiza barabara hiyo kwenye utaratibu wa kufanyiwa upembezi yakinifu na usanifu wa kina.

Hata hivyo amesema, barabara ya Mbambabay hadi Lituhi tayari imefanyiwa usanifu wa kina ili hatimaye ianze kujengwa kutokana na umuhimu wa barabara hiyo ambayo ni ya ulinzi na inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Njombe.

Pia amesema, tayari serikali imeifungua wilaya ya Nyasa kwa kujenga barabara ya lami nzito kilometa 66 kutoka Mbinga hadi Mbambabay iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 129.

Katika hatua nyingine Kasekenya amesema,serikali ya Awamu ya Sita imekamilisha ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu lenye urefu wa meta 100 linalounganisha wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma na wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

Aidha alisema,serikali inaendelea kujenga barabara ya Lami kipande cha kutoka Kitahi wilayani Mbinga hadi Ndumbi wilayani Nyasa ambako imejengwa bandari maarufu ya Ndumbi ambayo imekamilika kwa asilimia 100 na imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 12.

“Barabara ya Kitai hadi Ruanda kwa kiwango cha lami inaendelea kujengwa,pia serikali itaendelea kujenga barabara ya lami kutoka Ruanda-Lituhi hadi Ndumbi,Mkandarasi ameshapatikana barabara hiyo inaanza kujengwa kwa kiwango cha lami mwaka huu wa fedha’’,alisema Mhandisi Kasekenya.

Ameongeza kuwa serikali katika mwaka huu wa fedha imetoa shilingi bilioni 70 ili kuanza kujenga upya bandari ya Mbambabay wilayani Nyasa hali ambayo itaiunganisha wilaya ya Nyasa na nchi jirani za Malawi na Msumbiji kupitia ziwa Nyasa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Filberto Sanga ameishukuru serikali kwa kuifungua wilaya ya Nyasa kwa njia ya barabara na majini hali ambayo imemaliza kero ya usafiri na usafirishaji.

Amesema Wilaya ya Nyasa imefunguka kupitia ziwa Nyasa,serikali imejenga meli tatu mpya moja ya abiria ya MV Mbeya II na meli mbili za mizigo ya MV Njombe na MV Ruvuma zinazofanya kazi katika ziwa Nyasa kupitia bandari za wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya,Ludewa Mkoa wa Njombe na Nyasa Mkoa wa Ruvuma.

Munekano wa mji wa Mbambabay wilayani Nyasa baada ya serikali kuboresha miundombinu ya barabara na majini.

 



Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Filberto Sanga akiwa ofisini kwake mjini Mbambabay.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...