Na: Mwandishi Wetu - MANYARA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amemuagiza mkandarasi anayejenga uwanja wa mpira wa Kwaraa kumaliza kwa wakati ili kutumika katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.

Mhe. Katambi ametoa maelekezo hayo Agosti 11,2023 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwanja huo kuelekea kilele cha mbio hizo za zitakazohitimishwa Oktoba 14, 2023.

Aidha, amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo ni mpango wa Serikali katika kuwasongezea karibu viwanja vya michezo wananchi wa Mkoa wa Manyara lakini pia utakautumika kwenye kilele hicho.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Lazaro Twange amemhakikishia Naibu Waziri kuwa kuwa watamsimamia mkandarasi ili ujenzi huo ukamilike ndani ya muda uliopangwa.

Katiziara hiyo, Mhe. Katambi amekagua pia Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro -Manyara itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa, uwanja wa stendi ya zamani itakapofanyika wiki ya vijana na kukagua maendeleo ya vijana wa halaiki katika Shule ya Sekondari ya kutwa ya Babati. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akiangalia ramani ya mchoro wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa Kwaraa wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwanja huo tarehe 11 Agosti 2023 kuelekea kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Mkoani Manyara.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akikagua ujenzi wa uwanja wa Kwaraa akiwa ameambatana na Viongozi wa Mkoa wa Manyara pamoja wajumbe wa kamati ya maandalizi ya wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwanja huo tarehe 11 Agosti 2023 kuelekea kilele cha mbio hizo Mkoani Manyara.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akisisitiza jambo wakati akikagua maendeleo ya uwanja wa Kwaraa tarehe 11 Agosti 2023, kuelekea kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Mkoani Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Lazaro Twange (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakati akikagua maendeleo ya uwanja wa Kwaraa tarehe 11 Agosti 2023, kuelekea kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Mkoani Manyara.
Mkandarasi wa Uwanja huo, Mhandisi Theophan Rantaley (wa tatu kutoka kulia) akitoa taarifa ya hatua zilizofikiwa ujenzi wa Majukwaa wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kulia) alipotembelea uwanja huo Agosti 11, 2023 Mkoani Manyara.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU  (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...