Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhe Atupele Mwakibete (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya maonesho ya TCAA Mhe Atupele Mwakibete (Mb) ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya kilimo maarufu Nanenane yanayofanyika Kitaifa Jijini Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale na kutoa pongezi kwa TCAA kwa usimamizi dhabiti unaopelekea usafiri wa anga kuwa kiungo muhimu kwenye kilimo kwa kusafirisha bidhaa za kilimo kama mazao yanayoharibika haraka pamoja na namna teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani (drones) zinavyoleta mapinduzi katika kilimo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhe Atupele Mwakibete (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TCAA Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Songwe Fredy Mbele wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TCAA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhe Atupele Mwakibete (Mb) akizungumza na wafanyakazi wa TCAA wakati alipotembelea banda la TCAA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale , Jijini Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...