Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni kati ya Taasisi za Kiserikali zinazoshiriki Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima yanayotambulika kama NaneNane kwa ajili ya kutoa elimu ya majukumu ya shirika hilo.
Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Mbeya yameanza tarehe 1 Agosti na kilele chake ni tarehe 8 Agosti, 2023.Kauli mbiu ya maonesho hayo ni:- “Tanzania: Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo ya Chakula na Usalama wa Chakula ”.
TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanayotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.
Katika moja ya majukumu ya TASAC ni usalama wa vyombo vya usafiri majini ikiwemo, mitumbwi na meli ndogo za uvuvi ambayo ni moja kwa moja wanagusa wananchi kwenye sekta ya uvuvi kutoa elimu.
TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea banda la TASAC lipo katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Calvin akizungumza na wananchi mbalimbali hawapo pichani waliotembelea katika banda la TASAC kwenye maonesho Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John
Mwakangale jijini Mbeya.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Calvin akizungumza na wananchi mbalimbali hawapo pichani waliotembelea katika banda la TASAC kwenye maonesho Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John
Mwakangale jijini Mbeya.
Mwananchi akisaini kitabu na kutoa maoni yake juu ya majukumu ya TASAC wakati alipotembelea banda la TASAC Maonesho ya Kimataofa ya Kilimo kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...