Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete (MB), amekipongeza Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa kuendelea kutoa mafunzo ya Ubaharia kwa maendeleo ya Uchumi wa Bluu.
Mhe. Mwakibete amesema hayo alipotembelea kwenye banda la Chuo cha Bahari Dar es Salaam kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale vilivyopo Jijini Mbeya.
Chuo cha Bahari Dar es Salaam kinashiriki katika maonesho ya Nanenane 2023 jijini Mbeya ambapo huduma mbalimbali zinatolewa katika banda lao zikiwemo kutoa elimu ya ubaharia, elimu ya uokozi wakati wa dharula melini pamoja na usajili kwa wanafunzi wanaohitaji kujiunga na chuo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete akitia saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la DMI
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa watumishi wa DMI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...