Na Mwandishi Wetu, Same

WATU sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kuficha Kwa kuwahifadhi wahalifu walioingia kinyemela na kujihusisha na uchimbaji wa madini eneo ambalo ni chanzo cha maji  kinachotegemewa na wakazi zaidi ya 22,000.

Wakati wanaotegemea chanzo hicho ni  wa kata nne za Vudee,Mwembe,Mhezi na Mbangalala Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni matokeo ya Oparesheni ya kamati ya Usalama Wilaya ya Same iliyo ongozwa na Mwenyekiti wake ambae ni mkuu wa Wilaya Kasilda Mgeni.

Mgeni aliongoza operesheni hiyo ya kushtukiza baada ya kupata taarifa za kuwepo watu zaidi ya 70 wanaoendesha shughuli za uchimbaji madini Aina ya Dhahabu bila vibali.

Akieleza zaidi Mkuu wa Wilaya Mgeni amesema taarifa zilizopo mbali na wachimbaji hao kufanya shughuli zao kinyemela,  pia wameharibu miundombinu ya maji na kuhatarisha usalama wa watumiaji kwani wanasafisha madini moja kwa moja kwenye Bwawa wakitumia Mercury ambayo ni hatari kwa binadamu.

"Kuingia huku kinyemela na kuharibu miundombinu ya Maji NI hujuma, hatutavumilia vitendo kama hivi, niwatake Jeshi la Polisi kuweka kambi kwenye eneo hili kuimarisha ulinzi kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinakoma na waliohusika kuihujumu Serikali lazima watafute popote na wachukuliwe hatua."

Awali Kaimu Ofisa Mtendaji  kijiji cha Mteke Felix Ngeti amesema kwa sasa asilimia kubwa ya watu wamelazimika kuacha kutumia maji hayo kwakuwa uharibifu ni mkubwa  na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi kulazimika kutafuta huduma ya majinsafi maeneo ya mbali.

"Hapa mnapoona kuna wachimbaji zaidi ya sabini na viongozi wa kijiji walikuja baada ya kupata malalamiko kwa wananchi juu ya uchaguzi unaofanyika lakini wachimbaji hao kwakua waliokua wengi waliwafukuza viongozi, " amesema Ngeti.

Baadhi yao wakazi wanaoishi jirani na eneo hilo kulikofanyika uharibifu wamepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa huku wakielezs hali ilizidi kuwa mbaya na kumekua na ongezeko la idadi ya watu wanaingia kinyemela eneo hilo la chanzo cha maji na kuanza uchimbaji wa madini.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...