Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na linamuhoji kwa
kina Selemani Agai Gaya (18) mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya
Viongozi wakuu wa Serikali Tanzania kwa kutumia mitandao wa kijamii.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa huyu amekamatwa Julai 29, 2023.
"Mtuhumiwa huyu na wenzake wamekuwa wakitengeneza maudhui za mtandaoni (video) na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha viongozi wakuu wa Serikali katika akaunti zao za Tiktok.
"Mtuhumiwa huyu atafikishwa Mahakamani haraka
izekanavyo. Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu/ watu wanao toa lugha za matusi na fedheha
kwa viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote, " amesema.
Ameongeza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia
na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Julai 31, 2023 limewakamata watuhumiwa saba akiwemo Amani Kipolo mkazi wa
Vingunguti kwa tuhuma za kumshambulia na kusababishia kifo Hadija Hamisi na kuwajeruhi watu wengine nane.
Kamanda Murilo amesema watuhumiwa hao wakiwa na wenzao wakiwa kwenye kundi waliwashambulia
wananchi mtaani maeneo ya Vingunguti kwa lengo la kulipiza kisasi wakati
wakitoka kuzimka mwenzao aliyefahamika kwa jina la Nurdin Bwino.
Aidha, awali marehemu huyo Nurdin Bwino aliuwa kwa kushambuliwa na wananchi alipokuwa na wenzake sita wakiwa na visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia alipojaribu kuvunja nyumba moja usiku wa Julai 30, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...