Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa namna inavyotekeleza Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” (BBT – LIFE) na kuwataka vijana waliopo kwenye programu hiyo kutumia vyema fursa hiyo.

Rais Samia amesema hayo leo (08.08.2023) wakati alipotembelea mabanda ya wizara hiyo, kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yakiwa yanaelekea kuhitimishwa

Ameongeza kuwa amepata faraja kubwa kuona namna wizara hiyo ikiongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) pamoja na watendaji wa wizara wanavyosimamia vyema programu ya BBT – LIFE katika sekta za mifugo na uvuvi kwa kuwapatia vijana mafunzo ya vitendo ya unenepeshaji wa ng’ombe, kaa, jongoo bahari, pamoja na kilimo cha mwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...