Tuzo
hiyo imepokelewa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya Mhe. Rais,
wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa PSSSF,
kufuatia uamuzi wa Serikali wa kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya
PSPF, PPF, LAPF na GEPF, Agosti, 2018.
Akieleza
sababu za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kukabidhiwa tuzo hiyo, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce
Ndalichako, ambaye alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya PSSSF, alisema, Dkt. Samia
ni sehemu ya Mabadiliko hayo yaliyopelekea ufanisi katika utekelezaji wa
majukumu ya Mfuko.
“Tunamshukuru
kwa dhati, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa dhamira yake ya dhati kuhakikisha kwamba wastaafu wa nchi hii
hawapati usumbufu na hivyo kutoa fedha kiasi cha shilingi trilioni 2.17 katika
mfumo wa hati fungani ambazo kwa hakika zimeimarisha sana uwezo wa Mfuko
kuwahudumia Wanachama wakiwemo Wastaafu katika ulipaji wa Mafao kwa wakati.”
Alifafanua.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF) CPA. Hosea Kashimba amesema kuwa
katika kipindi cha miaka mitano, hadi kufikia Juni, 2023 mfuko huo umelipa
kiasi cha shilingi trilioni 8.88 kwa wanufaika 262,095.
Amesema
kuwa kati ya Julai, 2018 na Juni, 2023 mfuko huo umeweza kulinda na kuongeza
thamani yake kwa asilimia 27.76 kutoka trilioni 5.83 hadi trilioni 8.07 Juni,
2023. “Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 6.72 kwa kila mwaka”.
“Mhe.
Waziri Mkuu, hivi sasa kila mwezi tunalipa shilingi bilioni 67 kama pensheni
kwa wanufaika 164,828 na tunalipa kila ifikapo tarehe 25 ya mwezi husika bila
kuchelewa.” Alifafanua CP. Kashimba.
Na
sasa Mfuko unalipa Mafao ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria, alisisitiza
CPA. Kashimba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...