RAIS wa Shirikisho la Vyuo Vikuu kupitia Chama Cha Mapinduzi( CCM) Yunus Hassan Suleiman ametoa rai kwa watanzania hasa vijana kujiunga na Chuo cha Maendeleo ya Ujuzi, Ufundi na Viwanda( Furahika Education College) kilichopo Buguruni jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kupata ujuzi wa fani mbalimbali kutokana na kozi zinazofundishwa na chuo hicho.

Suleiman ameyasema hayo wakati wa mahafali ya kuaga wanafunzi 260 ambao wamehitimu kozi za Hotel Management, Ushonaji, Computer ICT, Secretaria, Upambaji, Urembo , Tourism pamoja na Clearing forwarding.

Aidha amewataka wazazi kuendelea kupeleka wanafunzi kwa ajili ya masomo ya kozi mbalimbali yanayotolewa katika Chuo hicho kwani kwa kufanya hivyo itakuwa sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk.Samia suluhu Hassan kwa kuwa chuo hicho kinatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)na hakuna chuo kama hicho nchini Tanzania.

Hivyo amewaomba viongozi wa Jumuiya ya Wazazi pamoja na Jumuiya ya Vijana kupeleka vijana kujiunga na chuo hicho kwa lengo la kupata ujuzi,lakini kuwasaidia vijana kujiepusha na dawa za kulevya na vitendo vya uhalifu kwa kuwa watakuwa na shughuli za kufanya kutokana na ujuzi walioupata.

Aidha amewaomba watumishi wa Serikali na viwanda vidogovidog kujiunga na kozi mbalimbali zinazofundishwa kwa njia ya mtandao(Online)ili kuendelea kujipatia ujuzi.

"Tunatoa rai kwa mashirika mbalimbali kuleta vijana wao na watumishi kujiunga na chuo hiki ambacho ni mfano wa kuigwa.Ni matarajio yetu mashirika kama World Vission, UNICEF, wataleta vijana wapate mafunzo, " amesema.

Ametumia nafasi hiyo kuipongeza Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kipawa, Kigamboni, Temeke, Tabata, Ilala, Kariakoo na Ubungo kwa kuunga mkono juhudi za Rais Samia huku akifafanua wanaotaka kujisajiri na chuo wanapaswa kuingia kwenye Website ya www.furahika.or.tz

Hata hivyo imeelezwa Chuo hicho kimeendelea kuwafikia watanzania walio wengi waliopo ndani na nje ya Tanzania kutokana na maboresho mapya ya mfumo mpya wa kujiunga hicho .

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...