Na. Lusungu Helela-Dar es Salaam
Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na Serikali ya Azerbaijan kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma bora na ya pamoja ‘‘One Stop Service Center” kwa wananchi kufuatia nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika eneo hilo.
Imeelezwa kuwa tangu nchi hiyo ilipoanza kutoa huduma hiyo ya pamoja kwa wananchi wake imesaidia tatizo la rushwa kuisha kabisa kwani uwezekano wa kuonana ana kwa ana kati ya wananchi na watoa huduma umepungua kwa kiasi kikubwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu ya Wakala wa Taifa kwa Utumishi wa Umma na Ubunifu wa Kijamii ya nchini Azerbaijan jijini Dar es Salaam.
“Mimi pamoja na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali tumefanya mazungumzo na timu ya wataalamu kutoka nchini Azerbaijan ambapo wametueleza jinsi walivyofanikiwa katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi wao ambapo na sisi tumewaelezea jinsi tunavyofanya maboresho mbalimbali katika eneo hilo’’ amesema Mhe. Simbachawene
Amefafanua kuwa Serikali imejipanga kuanzisha vituo 31 vya utoaji wa huduma kwa wananchi kupitia dirisha moja ambapo kwa kuanza kila mkoa utakuwa na kituo kimoja huku Jiji la Dar es Salam kutokana na uwingi wa watu litakuwa na vituo vitatu na Zanzibar kutakuwa na vituo viwili.
Amesema lengo la vituo hivyo ni kuhakikikisha Wananchi wanapata huduma za Serikali katika eneo moja hali itakayosaidia kupunguza mianya ya rushwa pamoja na ukiritimba.
‘‘Tunaamini kupitia kikao hiki cha kubadilishana uzoefu na wenzetu wa Azerbaijan, tutaboresha huduma zetu na wananchi watazifurahia’’ amesema Mhe. Simbachawene.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wakala wa Taifa kwa Utumishi wa Umma na Ubunifu wa Kijamii ya nchini Azerbaijan, Mhe. Ulvi Mehdiyev amesema nchi yao iko tayari kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha mifumo ya kidijitali inatumika katika utoaji huduma ya pamoja kwa wananchi kwa lengo la kuokoa muda wanaoupoteza katika kupata huduma za Serikali.
Mwenyekiti huyo, Ulvi Mehdiyev, amesema Tanzania ikianza kuutekeleza mfumo huo, tatizo la rushwa litaisha katika ofisi za Serikali, uzalishaji utaongezeka kwani wananchi watakuwa na muda mrefu wa kuzalisha badala ya kutumia muda huo kuzunguka kufuatilia huduma katika ofisi za Serikali pamoja na kasi ya wananchi kulipa kodi itaongezeka kufuatia huduma bora watakazozipata Serikalini.
Ujio wa Wataalamu hao kutoka nchini Azerbaijan ni matunda ya ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Mpango aliyoifanya mwezi Machi mwaka huu nchini humo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Wakala wa Taifa kwa Utumishi wa Umma na Ubunifu wa Kijamii ya nchini Azerbaijan, Mhe. Ulvi Mehdiyev mara baada kufanya mazungumzo ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza jijini Dar es Salam mara baada ya timu ya wataalamu wa Wakala wa Taifa kwa Utumishi wa Umma na Ubunifu wa Kijamii ya nchini Azerbaijan kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma bora na ya pamoja ‘‘ One Stop Service Center” kwa wananchi kufuatia nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika eneo hilo.
Sehemu ya timu ya wataalamu wa Wakala wa Taifa kwa Utumishi wa Umma na Ubunifu wa Kijamii ya nchini Azerbaijan wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa mazungumzo yaliyolenga kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma bora na ya pamoja ‘‘ One Stop Service Center ‘‘ kwa wananchi kufuatia nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Wakala wa Taifa kwa Utumishi wa Umma na Ubunifu wa Kijamii ya nchini Azerbaijan, Mhe. Ulvi Mehdiyev akizungumza jijini Dar es Salam mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kufanya kikao cha pamoja na timu ya wataalamu kutoka nchini Azerbaijan kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma bora na ya pamoja ‘‘ One Stop Service Center” kwa wananchi kufuatia nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika eneo hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na watalaamu kutoka nchini Azerbaijan pamoja na wataalamu wa hapa nchini mara baada ya kufanya kikao cha pamoja kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma bora na ya pamoja ‘‘ One Stop Service Center ‘‘ kwa wananchi kufuatia nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika eneo hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...