Na Immaculate Makilika - MAELEZO


Muelekeo wa Sekta ya Madini unalenga katika kuhakikisha Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa unafikia asilimia 10 au zaidi ifikapo mwaka 2025 kama inavyofafanuliwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa, Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 pamoja na Mpango Mkakati wa Tume ya Madini wa Mwaka 2019/2020-2023/2024.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 na mikakati ya mwaka 2023/2024.


“Katika kuhakikisha azma hiyo inafikiwa, Tume ya Madini inatarajia kuwa na mikakati ifuatayo ili kuwa na shughuli za madini ambazo ni endelevu za kuimarisha usimamizi na udhibiti katika maeneo ya uzalishaji wa madini ujenzi na madini ya viwandani kwa kuongeza Wakaguzi Wasaidizi wa Madini Ujenzi (AMAs), vitendea kazi (PoS) pamoja na kushirikisha Mamlaka nyingine za Serikali zinazosimamia na kutumia rasilimali hizi yaani Halmashauri, Polisi, TARURA & TANROADS, hii itasaidia kuuongezeka kwa makusanyo yatokanayo na rasilimali ya madini ujenzi na madini ya viwandani”, ameeleza Mhandisi Lwamo.


Mhandisi huyo ametaja baadhi ya mikakati kuwa ni kuimarisha udhibiti wa biashara haramu ya madini hususan utoroshaji wa madini kwa kuhamasisha umuhimu wa kutumia masoko na vituo vya madini nchini, kuimarisha vituo vya ukaguzi (exit-points) katika maeneo ya mipakani, bandarini pamoja na viwanja vya ndege kwa lengo la kusaidia kupungua kwa matukio ya utoroshaji wa madini na hivyo kuwezesha Serikali kupata takwimu sahihi na mapato stahiki.

Aidha, uboreshaji na usimamizi thabiti wa Mfumo wa Utoaji wa Leseni za madini utasaidia kupunguza migogoro itokanayo na muingiliano wa maombi ya leseni, kupunguza muda wa utoaji huduma pamoja na kuongeza idadi ya leseni zitakazotolewa kwa mwaka hivyo kuhamasisha uwekezaji.


Pia, Mhandisi Lwamo amesema kuwa kuimarisha ukaguzi katika shughuli za uchimbaji katika migodi kwa lengo la kuwa na uchimbaji endelevu unaozingatia usalama, afya na mazingira utasaidia kuongeza mapato, kuimarisha uchimbaji endelevu unaojali mazingira kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...