Farida Ramadhani, WF, Dodoma
Serikali
imeungana na nchi nyingine za Jumuiya ya Madola kwa kuanza kutumia
Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao utaboresha
upatikanaji wa taarifa za madeni.
Akizungumza jijini Dodoma
wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi.
Jenifa Omolo amesema mfumo huo utaleta tija katika kuhifadhi taarifa za
madeni pamoja na kuongeza uwazi wa takwimu za madeni hayo.
“Wizara
ya Fedha imeona ni muhimu kuingia kwenye mfumo mpya wa Kimataifa ambao
unatumiwa na wenzetu katika Jumuiya ya Madola”, alibainisha Bi. Omolo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mwandamizi wa Kurugenzi ya Uchumi, Vijana na
Maendeleo Endelevu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, Dkt. Ruth
Kattamuri, ambaye alishiriki uzinduzi huo kwa njia ya mtandao,
aliipongeza Serikali ya Tanzania kuingia katika mfumo huo na kuahidi
kuwa jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha
mfumo huo unafanya kazi kwa ufanisi na kuleta maendeleo.
Awali
akiulelezea mfumo huo, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni
kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, alisema mfumo huo
ulitengenezwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa mwaka
2019. Alisema Tanzania ilianza taratibu za kuhamia katika mfumo huo
kuanzia mwezi June 2022 kwa kutumia wataalam wa ndani.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akizungumza kabla ya
kuzindua rasmi Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao
Tanzania imejiunga rasmi ili kuboresha usimamizi wa taarifa za madeni,
jijini Dodoma.
Kamishna
Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama,
akizungumza kuhusu Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian),
katika uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Treasury Sruare, jijini
Dodoma.
Mkuu
wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleo na
Mshauri katika Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda, akizungumza kuhusu
Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), kabla ya kuzinduliwa
rasmi, jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akizungumza jambo na
Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw.
Omary Kama (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi,
Vijana na Maendeleo na Mshauri katika Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda
(kushoto), baada ya kuzinduliwa kwa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni
(CS-Meridian), jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (katikati), Meneja
MradiTaasisi ya Usimamizi wa Uchumi Mpana na Sekta ya Fedha Mashariki na
Kusini mwa Afrika (MEFMI), Bi. Josephine Tito (kulia) na Mkuu wa
Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleona Mshauri
wa Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda, wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, wajumbe kutoka Sekretariet ya Jumuiya
ya Madola, Serikali ya Zanzibar pamoja na Benki Kuu ya Tanzania baada
ya uzinduzi wa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), jijini
Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia
mawasilisho mbalimbali kabla ya kuzinduliwa kwa Mfumo mpya wa Usimamizi
wa Madeni (CS-Meridian), jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...