Maendeleo Benki imepongezwa na Serikali kwa kazi kubwa inayofanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maisha ya Watanzania yanaboreshwa Kiuchumi kwa kuwapatia Wafanyabiashara wadogo mikopo pamoja na kusaidia huduma za kiafya.

Pongezi hizo zimetolewa hapo jana Augost 1,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Edward Mpogolo wakati akizindua mbio za Maendeleo bank Marathon kwaajili ya kuchangisha fedha Kwa ajili ya kuboresha Kituo cha Watoto wenye changamoto ya akili.

Amesema Serikali itaendelea kuunga mkono sekta binafsi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inajari maendeleo ya watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw.Ibrahim Mwangalaba amesema kuwa  lengo la mbio hizo ni kutafuta shilingi milioni 200 ambazo zitafanya ukarabati na kununua Vifaa mbalimbali vinavyohitajika kwa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Kilele mbio hizo ni Septemba 2 mwaka huu ambapo Viongozi mbalimbali wa Kanisa na Serikali wataongozwa na mgeni rasmi ambaye anatarajia kuwa Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa na mbio hizo zinaongozwa na kauli mbiu inayosema hatua ya faraja.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...