Makandarasi wazawa wametakiwa kuzisimamia kampuni zao kwa ufasaha kwa kufuata sheria za ulipaji wa kodi kwa wakati na kufanya kazi kwa weledi kwa kutumia wataalamu stahiki katika sekta mbalimbali ili kukwepa changamoto katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo Makandarasi wazawa kibiashara, jijini Dodoma, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mha. Rhobin Nkori, alisema kuwa  lengo moja wapo la kufanya mafunzo hayo ni pamoja na kutoa elimu kwa makandarasi kuhusiana na mvutano baina yao na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).

“Nimefurahi kuona kwamba moja ya mada itakayofundishwa ni kuhusu masuala ya kodi kwa makandarasi, hii itatusaidia kupunguza  matatizo makubwa sana kati ya wakandarasi na TRA”, alisema Msajili.

Aidha Mha. Nkori, alisema makampuni mengine hutumika kufanya kazi kwa majina ya wamiliki wengine yanayopelekea mvutano pindi kazi inapoenda kukaguliwa na TRA kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi(CRB) hivyo amewataka wamiliki wa makampuni kusimamia vyema makampuni yao ili kuepuka changamoto hizo.

Mha. Nkori amesisitiza kuwa ili kuendelea kujenga taswira nzuri kwa makandarasi nchini, Bodi itaendelea kuwachukulia hatua kisheria makandarasi wote wanaokiuka maadili yao ya kazi.  

Naye, Mkurugenzi wa kampuni ya SONCO ENGINEERING COMPANY LIMITED, Mha. Baraka Materu, ameiomba serikali kuweka mikakati maalumu ya kuwashirikisha wakandarasi wazawa wakati wa utekelezaji wa miradi mikubwa ili kuwajengea uwezo makandarasi hao kutokana na teknolojia mpya ambayo watajifunza kupitia miradi hiyo.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanayotolewa na Bodi hiyo yameshirikisha makandarasi kutoka sehemu mbalimbali nchini lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo makandarasi hao katika mujukumu yao ya kazi.

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Rhoben Nkori, akizungumza na Makandarasi (hawapo pichani) waliokuwa kwenye mafunzo ya siku Tatu kuhusu masuala ya kibiashara kwa Makandarasi hao, Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakandarasi wakimsikiliza Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Rhoben Nkori (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku Tatu kuhusu masuala ya kibiashara kwa Makandarasi hao, Jijini Dodoma .

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Rhoben Nkori (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na makandarasi mara baada ya kufungua mafunzo ya kibiashara kwa makandarasi hao, yaliyofanyika jijini Dodoma.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...