Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Green Acres Bi. Jacqueline Rushaigo akizungumza na Waandishi wa habari pamoja na Wadau waliosoma shule ya Green Acres kuhusu maadhimisho ya miaka 23 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo. Kikao hicho cha maandalizi kilifanyika katika hotel ya Giraffe iliyopo eneo la Mbezi Africana Jumamosi iliyopita.

Na HIDAN RICCO.

Uongozi wa Shule ya Green Acres ulikutana na Wadau na Wanafunzi waliosoma shule hiyo miaka ya nyuma kujadili Mpango Mkakati wa kuendeleza shule hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa maadhimisho ya miaka 23 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2000.

Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo Bi. Jacqueline Rushaigo alieongoza kikao hicho kilichofanyika katika Hotel ya Giraffe iliyopo eneo la Mbezi Africana  aliwajulisha Waandishi wa Habari pamoja na Wadau waliohudhuria  kikao hicho kwamba shule hiyo inakusudia kuaandaa sherehe ya kuadhimisha miaka 23 tangu kuanzishwa kwake.

Akitoa historia fupi ya shule hiyo tangu ilipoanza rasmi mwaka 2000 ilipitia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafanikio ya kuongeza Matawi kadhaa kama vile Shule ya Green Acres Magomeni, mwaka 2008 na shule ya Bunazi Green Acres iliyopo mkoani Kagera ambayo ilianzishwa mwaka 2016.

Shule pia ilianza kupokea wanafunzi kutoka Nje ya Nchi, ukanda wa Afrika ya Mashariki mwaka 2003 na pia mwaka huo huo waliongeza Kidato cha 5 na 6 katika shule zao. Mwaka 2004 shule ya Green Acres walianzisha utaratibu wa ziara za Nje ya Nchi wakati wa Likizo na kutembelea Dubai katika Falme za Kiarabu pamoja na Pretoria na Johannesburn Nchini Afrika ya Kusini.

Shule ya Green Acres ilipata changamoto kidogo ya kushuka kwa viwango vya Elimu mwaka 2018 kufuatia kifo cha Muasisi wake na Muanzilishi wa shule hiyo Marehemu Julian Rushaigo Maarufu kama Mzee Bujugo ambaye pia alikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni.

Shule ya Green Acres ilipanda tena viwango vya Elimu  mwaka 2020 baada ya Shule ya Bunazi Green Acres ya Mkoani Kagera kushika nafasi ya 2 Bora Kitaifa upande wa Elimu, jambo ambalo limeongeza Tija na Sifa kwa Wazazi na Walezi kupeleka watoto wao katika shule hiyo.

Shule ina mandhari nzuri, Maabara za Kisasa ya masomo ya Sayansi na hivi sasa tunajenga Maabara nyingine ya Masuala ya Teknolojia ya Habari (Tehama) alisema Bi. Jacqueline Rushaigo Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na wanafunzi mbalimbali wake kwa waume waliosoma katika shule hiyo walitoa ushuhuda wa masuala mbalimbali yaliyowawezesha kupata Mafanikio makubwa katika Jamii.

Miaka 23 sio midogo, hivyo tupo katika maandalizi ya Maadhimisho maalum yatakayofanyika hapo baadae pia tumepanga kuwaalika Wadau mbalimbali tutakuwa na Mada maalumu pia na burudani zitakazo tolewa na Wasanii ambao wamesoma katika shule hiyo. Alisema Mkurugenzi Jacqueline Rushaigo.

Mmoja wa Msanii mashuhuri anaetamba na wimbo wake wa Enjoy kwa hivi sasa ni Juma Mussa Mkambala Maarufu kama JUX amesoma katika shule hiyo ya Green Acres na anatarajiwa atakuwepo katika Tamasha hilo. Alisema Mkurugenzi Mtendaji Bi. Jacqueline Rushaigo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...