Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid akipokea kipeperushi cha NACTVET kutoka kwa Mkurugenzi wa  Udhibiti Ubora wa NACTVE Dkt.Jofrey Oleke wakati alipotembelea Banda la NACTVET wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nne ya Elimu ya Juu yanayoendelea  Zanzibar kwenye viwanja vya Maisala , Zanzibar.

SPIKA wa Baraza la Wa wakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid, ameipongeza NACTVET kwa kushiriki maonesho ya 4 Elimu ya Juu yanayoendelea Zanzibar na kusisitiza NACTVET iendelee kutoa taarifa zenye tija katika masuala ya Elimu. Aidha, amehimiza utoaji elimu zaidi juu ya miongozo na taratibu za kujiunga na Vyuo kwani katika maonesho hayo ambayo ni fursa nzuri ya kukutana na wadau.

Mhe. Zubeir ametoa pongezi hizo leo 31Julai ,2023 alipotembelea banda la NACTVET akiwa ni mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa Maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Akiwa katika banda la NACTVET, Mhe. Zubeir amepatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora NACTVET, Dkt. Jofrey Oleke kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa NACTVET Dkt.Adolf Rutayuga, kuhusu majukumu ya NACTVET na inavyoshirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika kusaidia kuendesha vyuo vya kati vilivyopo kisiwani humo.

Aidha, Dkt. Oleke ameongeza kusema kuwa kwa upande wa Zanzibar NACTVET inasimamia Vyuo 17 vinavyotoa kada mbalimbali hivyo bado NACTVET inali jukumu kubwa la kuwafikia wadau zaidi kwa kutoa elimu mbalimbali kuhusiana na ujuzi.

Miongoni mwa wageni alioambatana nao Mgeni Rasmi ni pamoja Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Ali Abdul Gulam na Katibu Mkuu ,Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali, Mhe. Khamis Abdalla.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid akisani kitabu cha wagi wakati alipotembelea banda la NACTVET kwenye  ufunguzi wa maonesho ya Elimu ya Juu yanayoendelea Zanzibar , kwenye viwanja vya Maisala.

Baadhi ya picha mbalimbali za wananchi waliotembelea banda la NACTVET viwanja vya Maisala , Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...