Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imemfikisha mahakama ni afisa ugavi wa mji wa Geita Dorin Evarist Mushi na wenzie wawili afisa mtendaji wa Butundwe pamoja mzabuni kwa tuhuma za kuhujumu pesa za mfuko wa jimbo la Geita mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo mkuu wa Takukuru mkoa wa Geita Leonidas Felix alisema afisa ugavi huyo na wenzie wawili walidanganya kuwa wamepeleka tofali elfu tatu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Nyakagwe huku wakiwa wamepeleka tofali pungufu 1973 tu.

“kwahiyo hawa walikuwa na nia ovu tofali zilizokuwa zimesalia walikuwa wanaenda kuzifanyia tofauti na malengo yaliyokuwa yamepangwahivyo leo tutawafikisha mahakamani” alisema Leonidas

Aidha leonidas aliongeza kuwa pia TAKUKURU imewafikisha mahakamani watendaji watatu wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe kutumia pesa cha shilingi mili3.7 ambazo walikuwa wamekusanya na walizitumia kama fedha mbichi.

TAKUKURU katika kutekeleza majukumu yake pia imebaini mapungufu kwenye miradi 12 ambayo inagharimu kiasi cha shilingi bil 5.6 ambayo imeonesha viashiria vya rushwa na hatua zimeshachukuliwa.

Leonidas aliongeza kuwa TAKUKURU imejipanga kuendelea kutumia program ya TAKUKURU RAFIKI katika kuibua kero za wananchi ambazo zisipotatuliwa zinaweza kupelekea kuwepo kwa vitendo vya rushwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...