Na Mwandishi Wetu
Ikiwa ni sehemu ya kuwafikishia wakulima fursa mbali mbali ikiwamo mikopo ya riba nafuu, mafunzo na ushauri wa kitaalamu, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inashiriki maonesho ya wakulima ‘Nane Nane’ yanayofanyika jijini Mbeya kuanzia Agosti 1 hadi 8 mwaka huu.
Maadhimisho ya siku ya wakulima, Nane Nane, ambayo huenda sambamba na maonesho ya kilimo, hufanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wakulima kwa uchumi wa nchi. Maonesho hutoa pia fursa kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo kuonesha shughuli zao za kilimo kwa umma.
Meneja Mawasiliano na Masoko wa TADB Amani Nkurlu amesenma benki hiyo inashiriki maonyesho hayo makubwa ya kilimo kwa mara nyingine mwaka huu na kuwataka wakulima na wadau mbali mbali wa kilimo kufika katika banda lao kujifunza namna inavyosaidia sekta ya kilimo hapa nchini.
“Huu ni muendelezo wa TADB kushiriki maonesho ya Nane Nane kila mwaka. Kwetu sisi, maonesho haya ni muhimu sana kwa kuwa hutuwezesha kukutana moja kwa moja na wakulima na wadau mbali mbali wa kilimo kutoka kila kona ya nchi. Tunawakaribisha wakulima na umma kwa ujumla kutembelea banda letu lililopo kwenye viwanja vya John Mwakangale ili kujifunza kuhusu shughuli zetu na pia kujionea fursa mbali mbali,” alisema .
Aliongeza, “Kupitia TADB, wakulima wanaweza kupata mikopo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kwa riba nafuu zaidi katika soko hadi kufikia asilimia 9. Tunatoa huduma zetu kwa wakulima na wafanyabiashara katika sekta ya kilimo kwenye mnyororo mzima wa thamani ikiwemo sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi,” aliongeza Nkurlu.
TABD ilianzishwa mwaka 2015 kama taasisi ya kimaendeleo ya kifedha kwa lengo la kuchagiza mapinduzi ya kilimo Tanzania. Baadhi ya huduma za benki hiyo ni pamoja na mikopo ya Zana za kilimo, Mikopo ya Matrekta na mikopo kwa ajili ya miradi mbali mbali katika kilimo
Benki hii pia inatoa mikopo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) kwa kundi la wakulima wadogo kwa kushirikiana na mabenki washirika ya kibiashara ili kuhakikisha wakulima wadogo wengi zaidi wananufaika na mikopo ya riba nafuu, ambapo TADB inachukua jukumu la kutoa dhamana kwa wakulima hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...