Na Mwandishi wetu, Moshi


MBUNGE wa Bunge la Uingereza, Tracey Crouch anaendelea kupanda Mlima Kilimanjaro na leo amefika kituo cha Moyr Hut mita takriban 4,600 kutoka usawa wa bahari akibakiza vituo vitatu kufika kileleni na kuweka historia .

Crouch anapanda Mlima Kilimanjaro, akiwa na wanawake wenzake wanane kupitia kampuni ya Big Expedition and Safaris ya jijini Arusha na tangu ameanza kupanda amekuwa na furaha kubwa kupanda Mlima huku akifurahia kukaribia kileleni mwa Mlima Kilimanjaro.

Mbunge huyo ambaye yupo katika kampeni ya kuchangisha fedha kufanikisha matibabu ya saratani ya matiti kwa wagonjwa kesho anatarajiwa kufika kituo cha Baranko.


Crouch ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Michezo wa Uingereza kati ya mwaka 2017/18 anatarajiwa kushuka Mlimani Agosti 5 na kupokewa na wadau mbalimbali wa Utalii

kampuni ya kimataifa ya Utalii ya Uingereza ya Action Challenge kwa kushirikiana na Big Expedition and Safaris ndio wanampandisha kileleni Mbunge huyo na wenzake katika safari iliyopewa jina la Delux VIP ambapo wanaopanda mlima wanapewa huduma za viwango vya juu zaidi (VIP service).

Mbunge huyo, ameanza Julai 29,2023 kupanda mlima huo mrefu barani Afrika, kupitia njia ya Lemosho .

Mkurugenzi wa kampuni ya Big Expedition and Safaris, Angel Minja akizungumza na MAIPAC media amesema ujio wa Mbunge huyo wa Uingereza ni kazi nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya The Royal Tour.

"Wageni kama Hawa kuwapata sio rahisi hivyo tunampongeza Sana Mama Rais Samia kuendelea kutangaza Utalii wetu vizuri"amesema.

Minja pia ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii, Waziri Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu Dk Hassan Abbas na wasaidizi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kuboresha Utalii.

"Waziri wetu anafanya kazi nzuri na sisi kama wamiliki wa kampuni za Utalii tunampongeza na tunamuunga mkono"amesema.

Minja amesema kampuni yao ambayo mwaka huu imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa imekuwa na mafanikio hasa kutokana na kuweza kupokea wageni wengi maarufu Duniani.

"Sisi pia tunajitahidi sana kutoa huduma bora zenye viwango vya kimataifa na nzuri kwa wageni ndio sababu wageni maarufu Duniani wanapitia kampuni yetu ambayo ni ya wazawa," amesema.

Amesema hivi karibuni walipokea wageni ambao ni mabalozi wa Utalii kutoka nchini Uingereza lakini pia familia za watoto wa viongozi wakubwa katika Mataifa yaliyoendelea wamekuwa wakitumia kampuni yao.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...