Mganga mkuu wa serikali amesisitizia kutumika kwa takwimu sahihi na zenye ubora katika ufuatiliaji na udhibiti magonjwa mbalimbali yanapotokea hapa nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. TUmaini Nangu, wakati wa kuhitumisha mafunzo ya mpango wa kati wa mafunzo ya saba ya Epidemiolojia na maabara katika kituo cha elimu Masafa (CDE) Mganga Mkuu wa Mkoa Morogoro Dkt. Kusiryr Ukyoo amesema katika kufanya ufuatiliaji na udhibiti milipuko ya magonjwa kunahitajika kuzalisha wataalam wa kutosha katika halmashauri mikoa na taifa .

Aidha Dr Tumaini amesema kuwa matalajio ya serikali ni kuzalisha wataalam wa kutoshaa na kuimalisha mifumo ya afya

Mratibu wa Kituo cha Kudhibiti magonjwa nchini marekani Dr Andrew Makoi ambao wanaendesha program hiyo kwa kushirikiana na wizara ya afya na Chuo Kikuu Mzumbe amesema kuwa mpango huu umetoa mafanikio makubwa Kwa ajili ya kutatua changamoto na kuiomba serikali kuendeleza kutoa mafunzo Kwa wataalam zaidi.

Kwa Upande wake mganga mkuu mkoa wa Njombe Juma Mfanga amewasisitizia wataalam hao kutumia utalaam wao na kutambulika wanachokifanya ili kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla huku wahitimu wa mafunzo hayo Dr Uwezo Kinahi na Bi Lusia Yustas muuguzi kutoka wilaya ya Misenyi mkoani Kagera wakaelezea umuhimu wa elimu hiyo na namna itakavyowasaidia kubaini afua za awali za magonjwa ya mlipuko kwa kufanya ufuatiliaji na Kudhibiti.

Katika mafunzo hayo ya saba jumla ya wahitimu 25 wamehitimu mafunzo yao toka mikoa ya Rukwa,Mwanza,Ruvuma,Geita,Kagera na Njombe ambapo katika mafunzo hayo asilimia 75 ni mafunzo ya vitendo na asilimia 25 ikiwa ni mafunzo ya darasani mpango ulioanzishwa mwaka 2016 kwa ushirikiano wa serikali ya Marekani kupitia kituo cha Kudhibiti magonjwa(CDC)serikali ya Tanzania nchini ya wizara ya afya na Chuo Kikuu Mzumbe.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...