Farida Ramadhani, WF, Dodoma
Serikali imeungana na nchi nyingine za Jumuiya ya Madola kwa kuanza kutumia Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao utaboresha upatikanaji wa taarifa za madeni.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo amesema mfumo huo utaleta tija katika kuhifadhi taarifa za madeni pamoja na kuongeza uwazi wa takwimu za madeni hayo.
“Wizara ya Fedha imeona ni muhimu kuingia kwenye mfumo mpya wa Kimataifa ambao unatumiwa na wenzetu katika Jumuiya ya Madola”, alibainisha Bi. Omolo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwandamizi wa Kurugenzi ya Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, Dkt. Ruth Kattamuri, ambaye alishiriki uzinduzi huo kwa njia ya mtandao, aliipongeza Serikali ya Tanzania kuingia katika mfumo huo na kuahidi kuwa jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ufanisi na kuleta maendeleo.
Awali akiulelezea mfumo huo, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, alisema mfumo huo ulitengenezwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa mwaka 2019. Alisema Tanzania ilianza taratibu za kuhamia katika mfumo huo kuanzia mwezi June 2022 kwa kutumia wataalam wa ndani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akizungumza kabla ya kuzindua rasmi Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao Tanzania imejiunga rasmi ili kuboresha usimamizi wa taarifa za madeni, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, akizungumza kuhusu Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), katika uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Treasury Sruare, jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleo na Mshauri katika Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda, akizungumza kuhusu Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), kabla ya kuzinduliwa rasmi, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akizungumza jambo na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Omary Kama (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleo na Mshauri katika Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda (kushoto), baada ya kuzinduliwa kwa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (katikati), Meneja MradiTaasisi ya Usimamizi wa Uchumi Mpana na Sekta ya Fedha Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), Bi. Josephine Tito (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleona Mshauri wa Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, wajumbe kutoka Sekretariet ya Jumuiya ya Madola, Serikali ya Zanzibar pamoja na Benki Kuu ya Tanzania baada ya uzinduzi wa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mawasilisho mbalimbali kabla ya kuzinduliwa kwa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...