TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Kimataifa wa chakula Barani Afrika utakaofanyika kuanzia Agosti 10 hadi 12 jijini Dar es Salaam ambapo kampuni zaidi ya 500 zitashiriki kwa kuonesha bidhaa na kutoa huduma huku lengo kuu likiwa ni kufungua masoko ya kimataifa kwa mazao yanayozalishwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Hayo yameeelezwa na Mkurugenzi wa Mtandao wa mazao ya mikunde Tanzania (TPN,) Zirack Andrew alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza, kwa mara ya kwanza mkutano huo unafanyika Barani Afrika na Tanzania inakuwa mwenyeji wa mkutano huo ambao unatarajiwa kufungua soko la mazao ya chakula yanayozalishwa nchini kimataifa.

"Vyama mbalimbali vya mazao ya chakula Tanzania na Afrika vimeungana na kuwaalika wenzetu kutoka India ambao wamekuwa wazoefu wa kufanya mikutano na makongamano ya namna hii katika Nchi mbalimbali za Asia na Ulaya na kupitia mkutano huu tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuunganishwa katika masoko ya kimataifa." Amesema.

Amesema, katika mkutano huo kampuni zaidi ya 500 zitashiriki ikiwa ni pamoja na kuonesha bidhaa pamoja na washiriki 3000 ambao watatembelea mabanda na kupata huduma huku idadi hiyo ikijumuisha washiriki kutoka Nchi za Afrika na washiriki kutoka India, China, Ujerumani pamoja na Dubai.

Aidha ameeleza kuwa Nchi za Afrika zimekuwa zikizalisha mazao mengi bila kufahamu soko na Nchi zenye uhitaji hazina taarifa juu ya hazina ya chakula inayopatikana barani Afrika ikiwemo Tanzania na kupitia mkutano huo Nchi zenye uhitaji wa mazao ya chakula ikiwemo India, China na Afrika ya kati zitatumia fursa hiyo kwa kuwekeza na kufanya biashara.

Kwaupande wake Mtaalam wa Kilimo kutoka India Bw. Chandra Shekhar amesema, mkutano huo ni muhimu katika kuendelea kudumisha mahusiano mazuri ya kijamii na uchumi baina ya Tanzania na Nchi za Afrika kwa ujumla.

Ameeleza kuwa Afrika inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuingiza chakula nchini India na kwa miaka 10 ijayo nchi hiyo itaendelea kutegemea Bara la Afrika kwa ujumla katika suala la uingizaji mazao ya chakula.

"India na Afrika ikiwemo Tanzania tumekuwa na mahusiano mazuri ya kijamii na uchumi hususani katika kilimo na tumekuwa na changamoto zinazofanana ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa..na kupitia mkutano huu tutakutana na wakulima na wafanyabishara kwa lengo moja kila mmoja aweze kukua na kupeleka bidhaa katika soko la Kimataifa." Amesema.

Vilevile amesema kuwa mkutano utakuwa mwanzo wa taasisi za utafiti baina ya Tanzania na India kufanya kazi kwa pamoja katika kukabilina na changamoto zinazozikumba sekta ya kilimo pamoja na kutanua soko la kimataifa kwa mazao ya chakula yanayozalishwa Tanzania kimataifa ikiwemo India ambayo ina idadi ya watu ipatayo bilioni 1.35.

"Kupitia mkutano huu tutakutana na wajasiriamali wadogo katika sekta ya kilimo na tutawafundisha namna ya kufanya biashara kimataifa lengo likiwa ni kupunguza umaskini, kupongeza kipato pamoja na kutangaza bidhaa Kimataifa." Amesema.

Pia Mkurugenzi wa kampuni ya TASO kutoka India ambao ni waandaji wa mkutano huo kimataifa Suveer Rajpurohit amesema kuwa wamechagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na fursa nyingi zilizopo pamoja na kuvutia wawekezaji kuwekeza hususani katika kilimo.

" Asia, Ulaya na Amerika wamenufaika na mkutano huu na sasa tunazikutanisha Nchi 64 za Afrika hapa Tanzania, pamoja na nchi hizo kukuza soko la kimataifa la chakula pia zitavutia wawekezaji, wafanyabishara pamoja na kujitangaza Kimataifa." Ameeleza.

Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kuzinduliwa na Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara Tanzania, Dkt. Ashatu Kijaji utabeba mijadala mbalimbali ya kibiashara, semina, mawasilisho, kubadilishana uzoefu na ujuzi, tuzo na kuingia makubaliano ya kibiashara.
Mkurugenzi wa Mtandao wa mazao ya jamii ya kunde Tanzania (TNP,) Zirack Andrew (Kulia,) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa Kimataifa wa chakula barani Afrika na kueleza kuwa hiyo ni fursa kwa watanzania katika kutangaza bidhaa na kutafuta masoko ya mazao ya chakula kimataif jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa Kilimo kutoka India Bw. Chandra Shekhar (Katikati,) akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea mkutano huo na kuwataka vijana na wajasiriamali wadogo kushiriki na kutangaza bidhaa na huduma katika mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya TASO ambao ndio waandaji wa mkutano huo kimataifa Suveer Rajpurohit akizungumza kuelekea mkutano huo na kueleza kuwa wamechagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na fursa nyingi zilizopo na kuvutia wawekezaji hususani katika sekta ya kilimo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...