Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani kwa pamoja wamezindua kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwenye kaya ikiwa ni jitihada za pamoja katika mapambano dhidi ya malaria nchini Tanzania. Kupitia kampeni hii inayojitambulisha kwa jina la “Usingizi wa Starehe” itasambaza takribani vyandarua milioni 3.7 vyenye dawa katika kaya za Mkoa wa Kagera na Tabora.

Kupitia ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria (PMI), Serikali ya Marekani inafurahia kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Serikali ya Tanzania, pamoja na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa afua mbalimbali za malaria ikiwa na lengo la kuwalinda wananchi wake dhidi ya malaria na hivyo kuchangia katika kupunguza ugonjwa na vifo vitokanavyo na ugonjwa huu.

"Leo, tunasimama kwa pamoja katika dhamira yetu ya kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini Tanzania. Tunapozindua kampeni ya ugawaji vyandarua vyenye dawa katika kaya za mkoa wa Kagera na Tabora. Tunatambua ushiriki wa washirika wetu, ikiwa ni pamoja na Serikali ya Marekani, pamoja wadau wengine wa maendeleo, katika juhudi zetu za pamoja za kupambana na malaria,” amenukuliwa

Mheshimiwa Dkt, Godwin Mollel. Naibu Waziri wa Afya akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi. “Kwa kubadilisha vyandarua vilivyochakaa na kuhakikisha upatikanaji wa vyandarua vipya, tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya malaria na kulinda afya za jamii zetu.”

"Serikali ya Marekani inafurahi kuungana na wadau wetu wa malaria katika kuzindua kampeni hii ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa kwa jamii . Kwa kuhakikisha kuwa kaya zinapata vyandarua, na vyandarua hivi vinatumiwa kwa usahihi ili kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya malaria na kuwalinda watu walio katika mazingira hatarishi,” alisema Mshauri Mkazi wa Maswala ya Malaria kutoka USAID, Bi. Naomi Serbantez. "Kupitia kampeni hii, Marekani inasisitiza dhamira yake ya kuendelea kuisaidia Tanzania katika mapambano dhidi ya malaria na kuboresha afya na ustawi wa raia wake."Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...