Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufungua kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2023/2024 kuanzia leo Agosti 24 hadi Septemba 6, mwaka huu.

Pia tume imewasisitiza waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili ama kudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali kutumia fursa hiyo kwa kutuma maombi yao ya udahili kwa vyuo wanavyovipenda.

Katibu Mtendaji wa TCU, Prof.Charles Kihampa amesema hayo leo Agosti 25,2023 alipokuwa akitangaza kukamilika kwa udahili wa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza 2023/2024

Kufuatia kufunguliwa kwa awamu ya pili, tume pia imezielekeza taasisi za Elimu ya juu kutangaza programu ambazo bado zina nafasi huku waombaji wa vyuo pia wakihimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya pili.

“Waombaji na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyotolewa na TCU kama inavyooneshwa kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz)”. Amesema Prof.Kihampa.

Aidha Prof.Kihampa amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 116,133 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 80 vilivyoidhinishwa kudahili ambapo jumla ya programu 809 zimeruhusiwa kudahili ikiilinganishwa na programu 757 za mwaka 2022/2023 ikiwa ni ongezeko la programu 52 za masomo.

Amesema mwaka huu kuna jumla ya nafasi 186,289 ikilinganishwa na nafasi 172,168 kwa mwaka uliopita ikiwa ni ongezeko la nafasi 714,121 za shahada ya kwanza ambazo ni sawa na asilimia 8.2

"Katika awamu hii ya kwanza ya udahili jumla ya waombaji 86,,624 sawa na asilimia 74.6 wamepata udahili vyuoni, mwenendo huu wa udahili wa awamu ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitano (2019/2020 hadi 2023/2024) unaoonyesha ongezeko kubwa la waombaji ni ikiashiria ongezeko la wahitimu kidato cha sita na wale wa stashahada", amesema Prof.Kihampa.

Aidha Tume imewataka waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja kuthibitisha udahili wao kwa kuchagua chuo kimojawapo kuanzia leo Agosti 25 2023 hadi Septemba 6 2023 kwa kutumia namba zao za simu ama barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.

Pia TCU imewaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TCU) Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wahabari kuhusu kukamilika kwa dirisha la kwanza na kufunguliwa kwa dirisha la pili la udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/2024 leo Agosti 25,2023. jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...