Na Mwandishi wetu, Simanjiro


WAKULIMA wa Kata ya Msitu wa Tembo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameharibiwa ekari 28 za mazao yao ya mahindi baada ya tembo kuvamia kwenye mashamba yao.

Diwani wa kata ya Msitu wa Tembo, Kaleiya Mollel akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet ameiomba serikali ichukue hatua.

Mollel amesema tembo hao wamevamia mazao ya wananchi wake na kuharibu mazao yao hivyo kusababisha wakulima kupata hasara kupitia ekari 28 za mahindi.

"Tembo hawatosheki hata ekari 500 haziwatoashi sasa ili kubakiza kile kilicholimwa tunaomba tembo hao waondolewe kwenye eneo la kata yetu," amesema Mollel.

Amesema serikali iingilie kati suala hilo kwani wakulima watakumbwa na njaa na kuomba msaada serikali kwani hakutakuwa na mavuno.

Hata hivyo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Gracian Makota amekiri kuwepo kwa tembo kwenye baadhi ya kata.

"Tupo kwenye mpango wa kumaliza kero na changamoto hiyo ya tembo kwa kuwafundisha wana vijiji namna ya kuwafukuza mashambani tembo hao," amesema Makota.

Kwa upande wake kaimu ofisa maliasili halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Joseph Shamba amesema wameandaa mpango wa kuwafundisha vijana wa maeneo husiika ili wawafukuze tembo hao.

Shamba amesema kata zenye changamoto kubwa waandae vijana 10 au 30 kwenye vijijini ili watengeneze mabomu kupitia fataki na tochi zenye mwanga mkali.

"Tunaanza na kata za Msitu wa Tembo, Loiborsoit, Ngorika na Edonyongijape kwani ndizo zimeathirika mno kisha maeneo mengine yatafuata," amesema Shamba.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...