Na Mwandishi Wetu

BOHARI ya Dawa (MSD) imeingia mkataba na kampuni ya Hainnan International kwa ajili ya ujenzi wa maghala ya kisasa (WiB)kwa ajili ya uhifadhi wa bidhaaa za afya, Kanda ya MSD Dodoma.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mradi huo, Meneja Miradi wa MSD, Deo Orauya ameeleza maghala hayo yatakua kitovu (hub) cha uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya kwenye Kanda nyingine za MSD hasa zinazohudumia Kanda ya Kati, Kanda ya Magaharibi, na Nyanda za Juu Kusini.

Amefafanua kutokana na ongezeko la watu na ujenzi vituo vipya vya kutolea huduma za afya nchini, MSD imejidhatiti kuongeza uwezo wake wa uhifadhi, ili kuendana na mabadiliko hayo kwa kujenga maghala ya kisasa, ambapo pia utasaidia uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya nchini.

Pamoja na hayo amesema makabidhiano ya eneo la ujenzi, yameongozwa na mshauri mwelekezi Architect Nkini kutoka kampuni ya ABECC, inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi -Dar es Salaam.

Ujenzi wa maghala hayo yenye ukubwa wa sqm elfu 5, katika kiwanja na.92/1&2/Kizota Dodoma, jirani na Ofisi za Kanda za MSD, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 10, huku ikiakisiwa huenda ujenzi ukakamilika ndani ya muda mfupi zaidi ya huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...