Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati wa Kufungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii kijinsia katika muktadha wa utoaji huduma za misingi ya Haki za Binadamu kupitia hatua mbalimbali jijini Dar es Salaam leo hayo leo Agosti 07, 2023.
Mwezeshaji, Nemes Mabung’ai akizungumza na wawakilishi wa Asasi za wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii kijinsia katika muktadha wa utoaji huduma za misingi ya Haki za Binadamu kupitia hatua mbalimbali jijini Dar es Salaam leo hayo leo Agosti 07, 2023.


Baadhi ya Wawakilishi wa Asasi za Kiraia wakiwa kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na TGNP jijini Dar es Salaam leo Agosti, 07, 2023.


Na Avila Kakingo, blog ya Jamii
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) wawajengea na kuimarisha uwezo wa Wawakilishi wa asasi za kiraia zilizo katika mitandao yote ya TGNP ikiwa ni pamoja na wanavituo vya taarifa na maarifa na wanaharakati wengine ngazi ya Jamii.

Akizungumza wakati wa Kufungua Mafunzo hayo leo Agosti 07, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amesema kuwa wanawajengea uwezo juu ya dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii kijinsia katika muktadha wa utoaji huduma za misingi ya Haki za Binadamu kupitia hatua mbalimbali.

Akielezea hatua hizo Mkurugenzi huyo amesema Mpango na Mgawanyo wa Rasilimali, Usimamizi wa Matumizi, Usimamizi wa Ufanisi au Utendaji, Uadilifu wa Umma na Usimamizi wa Uwajibikaji au Utendaji.

“Kujenga uelewa wa pamoja kwa mashirika yanayotetea haki za wanawake, mitandao ya wanawake, wawezeshaji na wanaharakati ngazi ya jamii juu ya dhana muhimu zinazotumika kwenye ufuatiliaji wa uwajibikaji Jamii kwa mtizamo wa kijinsia.” Amesema Lilian

Amesema mafunzo hayo pia yatawajengea uwezo wa kutengeneza mwongozo na mbinu bora za ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii kwa mtizamo wa kijinsia pia kutengeneza mikakati ya namna ya kuwa na mifumo thabiti ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamiii katika mtizamo wa kijinsia ili kuimarisha taasisi zenye mifumo bora ya kuhakikisha kuna ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii hususani utoaji wa huduma kwenye jamii.

Amesema kwa miaka 30 sasa, TGNP wamekuwa mstari wa mbele katika kujenga uwezo na ushawishi juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia pia kujihusisha na mchakato wa bajeti kila mwaka kwa kuwawezesha wanawake na makundi yaliyo pembezoni katika ngazi za jamii kushiriki kikamilifu kupitia mchakato wa fursa na vikwazo (O&OD) unaofanyika katika ngazi ya jamii ili kuweza kuibua vipaumbele.

Kupitia hayo Lilian amesema kuwa Mafunzo hayo yatawaunganisha na kuibua mjadala wa kitaifa ili kudai utengwaji wa rasilimali kwa ajili ya masuala ya jamii kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusiana na maeneo ambayo tuwamekuwa wakiyafanyia uchechemuzi ili yatengewe bajeti ni pamoja na elimu, afya, kilimo, maji, haki ya mazingira na uwezeshaji kiuchumi.

Pia amesema ufuatiliaji wa bajeti yenye mrengo wa jinsia ni muhimu kwaajili ya kuhakikisha yale wanayoyapigania yanafanyiwa kazi, kutengewa bajeti lakini pia kutumika kama ilivyokusudiwa.

Kwa Upande wa Mwezeshaji, Nemes Mabung’ai amesema kuwa Asasi za Kiraia hapa nchini zinachangamoto ya vitendea kazi pamoja na Rasilimali fedha na rasilimali watu ambao wanaweza kutembelea maeneo ya vijijini kukusanya data ili usimamizi wa rasilimali za serikali katika utimizaji wa majukumu.

Pia amesema serikali inapanga bajetI kulingana na mfadhili anayetoa fedha kwaajili ya maendeleo. Pia ametoolea mfano kuwa Wizara ya Afya mara nyingi ndio inapanga bajeti kulingana na vipaumbele vya mfadhili na sio vipaumbele vya jamii husika.

Amesema bajeti ya serikali na utekelezaji wake hauendi sambamba na mahitaji ya Wanawake, Walemavu, Wanaume, Vijana, Watoto… lakini unatenga bajeti kwa ujumla bila kujali akinamama wanaojifungua. Pia ametolea mfano kuwa akinamama wanaambiwa waende na vitu vya kujifungulia ingali bajeti ya serikali imetenga bajeti ya Wizara ya Afya.

Mabung’ai ametoa rai kwa serikali kutenga bajeti yenye jicho la kijinsia ili kila mmoja anufaike na kodi anayoitoa pia isiwe na vipaumbele tofauti na vipaumbele vya jamii.

Kwa Upande wa Mnufaika wa Mafunzo hayoCatherine Kalinga kutoka Shinyanga amewashukuru TGNP kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatawajengea uwezo wa kupata mbinu zitakazo wasaidia kukusanya maoni, data na kupima namna gani bajeti ya serikali inatumika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...