Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, ametembelea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwenye maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kuipongeza benki hiyo kwa kuwahudumia wakulima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Frank Nyabundege alimwambia Katibu Mkuu Kiongozi kuwa TADB imeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608.5 ambayo imewanufaisha wakopaji 1,657,544.
Nyabundege alisema benki hiyo imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya kusaidia mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (Building a Better Tomorrow – BBT) iliyo chini ya Wizara ya Kilimo. Pamoja na hayo, alisema kuwa benki imetenga shilingi bilioni 8 kama mkopo kwa vijana na wanawake ambazo zitakwenda kuwakopesha wahitimu wa mradi wa BBT kwa riba nafuu.
“TADB imetenga shilingi bilioni 8 kupitia programu maalumu ya mikopo kwa wanawake na vijana, ambayo kwa kuanzia, benki itaanza kuwakopesha wahitimu wa BBT watakaofanya shughuli zao za kilimo kwenye shamba ya vitalu, Chinangali, Dodoma,” alisema Nyabundege.
Kwa maelezo ya Nyabundege, mchango wa TADB katika kuwainua wanawake na vijana katika kilimo ni wa muhimu tukizingatia ya kwamba kauli mbiu ya Nanenane mwaka huu unasema “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo ya usalama wa chakula” .
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya Nane nane yanayoendelea jijini Mbeya.
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya Nane nane yanayoendelea jijini Mbeya. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa TADB na ujumbe ulioambata na katibu mkuu kiongozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...